Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Omari Mgumba akiwa na kamati ya ulinzi Wilaya ya Korogwe alipokwenda kukagua miradi ya maendeleo.
*******************
Na Hamida Kamchalla, KOROGWE.
SERIKALI nchini imepanga kufanya mradi mkubwa wa kuboresha miundombinu ya elimu msingi baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uboreshaji kwa Elimu sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba ameyasema hayo mbele ya kamati ya ulinzi Wilaya ya Korogwe, kwamba mafanikio yaliyojitokeza katika maboresho hayo yameleta tija kwa serikali na kuhamasika kuja na mpango wa mradi huo katika elimu msingi.
"Kuanzia mwezi wa kwanza, kutokana na jitihada hizo, ataendelea kuanza mradi mkubwa kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya elimu kwa shule za msingi, nimekuja kuwapa habari hizi njema, lengo likiwa tujiandae".
"Kwa maana ya kwamba, ni vizuri tukafanya tathimini ya kina kujua kwamba hali za shule zetu katika maeneo yetu zikoje, shule gani inatakiwa maboresho, idadi ya wanafunzi pamoja na mengine yaliyomo ndani ya shule za msingi, shule zipi zirekebishwe au kubomolewa kabisa au hata eneo kuanzishwa shule mpya kutokana na ongezeko la wanafunzi" ameeleza.
0 Comments