Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS KUONGOZA KONGAMANO LA WAHARIRI NA WANAHABARI KUHUSU UHIFADHI WA MAZINGIRA NA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI DESEMBA 19, 2022 IRINGA



************************


Disemba 19 2022 Makamu wa Rais Dk. Philip Isdor Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji, litakalohusisha Wahariri na Wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Digitali, Blog, Redio, Televisheni, na Magazeti; Mawaziri, Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mashirika ya umma, Mashirika ya kimataifa, na Wadau mbalimbali wa uhifadhi na utunzaji wa mazingira kujadili na kutafuta suluhu ya hali inayoendelea ya uharibifu wa mazingira nchini kongamano litakalofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Mkwawa Iringa.


Akizungumza Desemba 11 katika mkutano na Waandishi wa habari Dar es Salaam, Mwenyekiti wa MECIRA, Habibu Mchange, amesema kituo hicho kimeamua kuvalia njuga uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kulifanya suala hilo kuwa endelevu na kusema kuwa kumekuwapo mijadala mingi juu ya ukosefu wa umeme wa uhakika, uhaba wa maji,kuchelewa kwa vipindi vya mvua, kuongezeka kwa joto lakini Watanzania hawaelezwi ukweli juu ya uharibifu mkubwa unaofanyika katika vyanzo vya maji unaosababishwa na shughuli za kibinadamu.


“Hali ni mbaya, yanayofanyika huko ni mambo ya ovyo ambayo yanapaswa kupigwa kelele. Sisi wanahabari tunapaswa kueleza haya kabla hatujailaumu Serikali. Kalamu zetu ziwe tayari kueleza kwa kina juu ya uharibifu mkubwa wa mazingira na namna ya kuukabili,’’ amesema


‘’kwa mfano leo ni siku ya 126 mto Ruaha umekauka, hautiririshi maji, mabwawa kama mtera na kidatu yanategemea maji kutoka Ruaha ambayo haitiririshi maji, unapotokea mgao wa umeme wananchi watailaumu serikali, watamlaumu waziri, watamlaumu Rais, lakini tatizo sio wao tatizo ni uharibifu wa Mazingira.


Kwa upande wake, mjumbe wa MECIRA, Manyerere Jackton, amesema sasa ni wakati wa kuufanya uhifadhi wa mazingira, na utunzaji vyanzo vya maji kuwa endelevu na kwamba unahitajika utashi wa kisiasa, na kuishukuru Serikali kwa kujipambanua wazi katika hilo kupitia hotuba za viongozi wakuu wa Nchi, Rais, Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu huku alielezea masikitiko yake kwa aliyoyashuhudia alipotembelea mto Ruaha hivi karibuni.

Post a Comment

0 Comments