Ticker

6/recent/ticker-posts

MAYELE ANAZIDI KUWAFURAHISHA WANANCHI, YANGA IKIIBAMIZA 3-0 COASTAL UNIONS


NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Yanga imefanikiwa kuichapa Coastal Unions Fc kwa mabao 3-0, mechi ambayo imepigwa katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Fiston Kalala Mayele mnamo dakika 28 kipindi cha kwanza na dakika ya 47 kipindi cha pili, wakati bao la tatu likifungwa na Feisal Salum.

Ushindi huo wa Yanga sc umewafanya kuwaweka nafasi nzuri ya juu wakiwa na pointi 44 huku wapinzani wao Simba Sc akiwa nafasi ya pili akiwa na pointi 38 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Fiston Kalala Mayele ameendelea kuwa mwiba baada ya leo kufanikiwa kupachika mabao mawili nakufikisha mabao 13 wakati anaemfuata Moses Phiri akiwa na magoli 10.

Post a Comment

0 Comments