Ticker

6/recent/ticker-posts

RC SENYAMULE AKABIDHI ZAWADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akikabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya katika kituo cha Safina kilichopo Ntyuka Jijini Dodoma kwa niaba ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watoto katika kipindi cha sikukuu.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na walezi na Watoto wa kituo cha Safina kilichopo Ntyuka Mkoani Dodoma mara baada ya kukabidhiwa zawadi mbalimbali za sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Desemba 24, 2022.

********************

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule leo tarehe 24 Desemba 2022 amekabidhi zawadi mbalimbali za sikukuu za Krismasi na mwaka mpya katika kituo cha Safina kilichopo Ntyuka Jijini Dodoma kwa niaba ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Mchele, Unga wa Ngano, Sabuni, Sukari, Mafuta, vinywaji pamoja na mbuzi wawili. Amesema zawadi hizo ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watoto katika kipindi hiki cha sikukuu.

Amesema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuma salamu za Upendo na kuwaomba watoto hao kukua katika maadili ya kumpendeza Mungu na wanadamu.

“Lengo na dhumuni la Mhe. Rais ni kuona watoto wanasheherekea sikukuu kwa furaha na amani, kumbukeni kuwa chochote anachokifanya ni kwaajili ya watanzania wote ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa ili watoto mpate elimu bora na kuongeza kiwango cha utafulu, hivyo mkiwa darasani msikilize mwalimu na mkirudi kituoni muda wa jioni jisomeeni” Alisisitiza Mhe. Senyamule.

“Chochote unachokifanya fanya kwa bidii kila mtoto ana ndoto na malengo yake ya baadae, Serikali inatambua mchango wenu ndio maana Dkt. Samia Suluhu Hassan ameamua kutoa zawadi hizi za vyakula na kiasi cha fedha ili wote mfurahie sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya. Mhe. Senyamule aliongezea.

Mhe. Senyamule amewashukuru waangalizi wa watoto hao kwa kujitoa kwao kuwalea katika maadili mema na kumuomba Mungu kuendelea kuwabariki Walezi na wahudumu wengine katika malezi ya watoto hao.

“Jukumu lenu ni pamoja na kuhakikisha watoto hawa wasoma ili kuyatumia madarasa yanayojengwa na Serikali chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili tuwe na kizazi chenye maadili mema ya kitanzania na ndoto za kutimiza malengo ya watoto wetu” Alifafanua Mhe. Senyamule.

Aidha mlezi wa kituo cha Safina Bi. Neckson William ameishukuru Serikali kwa kutoa zawadi za sikukuu kwa watoto.

“Tunaishukuru Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutusaidia kituo cha Safina tumefurahi sana kwakuwa tuna watoto ambao pia wapo nje ya Safina. Kituo kinawatoto kuanzia miaka miwili na mwaka huu tumefanikwa kupeleka Chuo Kikuu watoto wawili” Alisisitiza Bi. William

Kituo cha Safina kilianzishwa mwaka 2004 na kina jumla ya watoto 40, wavulana 35 na wasichana 5 pia kitua hicho kinawasaidia watoto ambao wanatoka katika mazingira magumu.

Post a Comment

0 Comments