Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI 114,647 KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MDOGO KESHO

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na vyombo vya habari hii leo wakati akizungumzia maandalizi uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Amani, Mkoa wa Mjini Zanzibar na Udiwani katika kata saba za Tanzania Bara.


***********


Na Mwandishi Maalum

JUMLA ya Wapiga Kura 114,647 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Amani Mkoa wa Mjini, Zanzibar na Kata saba za Tanzania Bara hii kesho Desemba 17,2022.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele katika Risala ya Uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 17 Desemba, 2022 na kusema kuwa vituo vituo 289 vya kupigia kura vitatumika.

Post a Comment

0 Comments