Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MABULA ATOA SIKU 14 MAKAMPUNI YA UPIMAJI KUKWAMUA ZOEZI LA URASIMISHAJI VIWANJA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula pamoja na viongozi wa Manispaa ya Temeke wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliofika viwanja vya Shule ya Msingi Mabagala kuu Kuchukua hati zao mara baada ya kukamilisha taratibu za urasimishaji viwanja vyao. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akimkabizi hati Mkazi wa Mbagala Kuu Manispaa ya Temeke Bi. Rashida Azizi Mgaya hati tano alizokabidhiwa baada ya kukamilisha urasimishaji wa viwanja vyake jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Mabagala Kuu. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dr. Angeline Mabula akisoma maelezo ya hati kabla ya kuanza zoezi la utoaji hati jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Mabagala Kuu jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dr. Angeline Mabula akiongea na wananchi waliofika katika viwanja vya shule ya Msingi Mbagala Kuu Jijini Dar es Salaam kushuhudia zoezi la utoaji hati jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Mabagala Kuu jijini Dar es Salaam.

*******************

Na Anthony Ishengoma

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula ametoa siku 14 kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam kukaa na makampuni ya Upimaji Ardhi Mkoani humo ili kujiweka sawa kuhakikisha zoezi la urasimishaji Jijini Dar es Salaam linakwamuliwa kwani muda uliopangwa kwa kazi hiyo unakaribia kufikia tamati.

Waziri Mabula alisema hayo katika Viwanja vya Mbagala Kuu Jijini Dar es Salaam jana nakuonya kuwa makampuni ya urasimishaji na upimaji wa viwanja ambayo yamechukua fedha za wananchi na kushindwa kukamilisha zoezi hilo yatatakiwa kurudisha madeni lakini pia kufutwa ili iwe funzo kwa makapuni mengine ambayo yanafanya kazi kinyume na taratibu na kushindwa kufikia malengo.

Aidha Waziri Mabula amemtaka Mkurugenzi Manispaa ya Temeke pamoja na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Dar es Salaam kuhakikisha maombi yote ya hati ambayo wananchi wamewasilisha pamoja na kukamilisha malipo yawe yamefanyiwa kazi na wananchi wamepatiwa hati zao ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dr. Angeline Mabura ameziagiza Halmashauri zote Nchini ambazo ni mamlaka za upangaji ardhi nchini kuhakikisha zinatenga fedha kwa ajili ya kupima kupanga na kumilikisha ardhi badala ya kuachia sula hilo kubaki ni mzigo kwa Wizara wakati ni majukumu ya Halmashauri kufanya kazi hiyo.

Waziri Mabula pia amepiga marufuku kwa Mkoa wa Dar es Salaam kuendelea kutoa hati zinazozalishwa kwa njia ya analogia kwa wakazi wa Jiji hilo na badala yake watoe hati za kidijiti kwani mfumo wa ILMIS unafanya kazi lakini pia akawataka kuendelea kuhuisha kanzi data za ardhi katika mfumo wa kidijitali na kuzitaka Halmashauri nyingine nchini kuendelea na zoezi hilo.

Aidha Dkt. Mabula ameonya wale wote wanaoendelea na uvamizi katika maeneo ya watu bila Kwenda Ofisi za Halmashauri nchini kujiridhisha kuwa wanatenda kosa la jinai na kuonya watendaji kata na vijiji kuacha kuuza ardhi kwani hilo sio jukumu lao bali wenye mamlaka hiyo ni Ofisi za Halmashauri.

Dkt. Mabula ameongeza kuwa wananchi lazima wafuate sheria za ardhi zilizopo na kuonya kuwa kuna baadhi ya watu waliofanya uvamizi na wakatakiwa kulipa mwenye eneo lake lakini wameshindwa kufanya hivyo kwa mantiki hiyo sheria zitafuatwa na kuhakikisha wanatolewa katika maeneo hayo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndata Ludigija aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke katika hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kushiriki zoezi la utoaji hati kwa wananchi hao amesema kuna watu wanapoteza umiliki kutokana na kutopima ardhi suala linalopelekea migogoro ya ardhi kwani kuna baadhi ya wananchi hapa Nchini wakijua eneo halina hati wanatengeneza Nyaraka feki na kupora mari za wananchi.

Wakati huo huo Kamishna Msaidizi wa Jiji la Dar es Salaam Bw. Shukrani Kyando amesema zoezi la urasimishaji Jijini Dar es Salaam bado linakabiliwa na Changamoto ya uelewa mdogo wa wananchi kuhusu suala la urasimishaji lakini pia baadhi ya makampuni yanategemea michango ya wananchi hivyo kushindwa kuendesha zoezi la urasimishaji kama ilivyopangwa.

Post a Comment

0 Comments