Ticker

6/recent/ticker-posts

AHUKUMIWA KWENDA JELA MWAKA MMOJA NA FAINI YA SH. 2MILIONI KWA KUGHUSHI NYARAKA ZA SERIKALI


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemtia hatiani mshitakiwa Bi. Esther Peter Riwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Maendeleo ya Vijana iliyokuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika shauri namba 165/2019.

Mshitakiwa ameshtakiwa kwa kosa la kutumia nyaraka za kughushi katika kufanya marejesho ya masurufu kinyume na vifungu 333,335 & 337 Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 16 rejeo la Mwaka 2019.

Mahakama imemhukumu mshitakiwa huyo kulipa faini ya sh. 2,900,000/- au kifungo cha mwaka mmoja gerezani na imeamuru kurudisha kiasi cha sh. 2,900,000/- alizofanyia ubadhirifu.

Post a Comment

0 Comments