Ticker

6/recent/ticker-posts

CCM TANGA YAPANIA KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA KWA ASILIMIA ZOTE.

Mwenyekiti akiongelea utekelezaji wa katiba ya Ccm katika utekelezaji wa miaka mitano ndani ya uongozi wake.
Mwenyekiti akiwa na viongozi wengine wa chama Mkoa.

Baadhi ya viongozi wa Ccm Mkoa wakimsikiliza mwenyekiti.


***********************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

CHAMA cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Tanga kimedhamiria kufanya utekelezaji wa ilani ya chama kwa asilimia kubwa katika kila nyanja ili kuhakikisha wanatoa hamasa kwa wananchi wote mkoani humo wanachama na wasio wanachama wanajiunga na chama hicho katika utekelezaji wake.


Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Tanga Rajabu Abdalla amesema hayo wakati akikabidhiwa ofisi rasmi kuanza kazi ambapo alisisitiza kuwa kila kiongozi kwa nafasi yake ahakikishe anaeajibika katika utekelezaji wa ilani hiyo ili kubadili mtazamo hasi kwa baadhi wa watu.


Amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo ya uongozi wake kwa kushirikiana na viongozi wengine na wanachama wa Ccm anataka kukijenga chama ili kiwe kimbilio la wanyonge wote katika Mkoa wa Tanga.


"Kwa mfano tulioufanya Wilaya ya Kilindi nikiongoza kamati ya siasa katika kutatua mgogoro wa ardhi kabla sijaripoti ofisini, tunaposema tunahitaji chama kiwe kimbilio la wanyonge huwa tunamaanishandiyo chama kinachotakiwa kiwe tangu kuasisiwa kwake" amesema.


"Tunapoona wanyonge hawana mahala pa kusema matatizo yao ni lazima tuwakimbilie ili watoe yao ya moyoni kupitia chama chetu, kwahiyo ndani ya miaka mitano ya uongozi wangu nataka chama kiwe kimbilio la wanyonge wote katika Mkoa wa Tanga, na hakitambagua mtu yeyote kwa unyonge au utajiri wake" amesisitiza.


Aidha amebainisha kwamba chama kitahakikisha kinaendelea kutekeleza ilani yake ipasavyo kwa kuzingatia yale yote walitoyaahidi wakati wa uchagu mkuu wa mwaka 2020 yanatimia ili itakapofika wakati wa uchaguzi mwengine wa 2025 wananchi wasiwe na hoja za kuweza kuwakwamisha.


"Lakini mimi, nimerithi kijiti hiki na kukuta Tanga Ina migogoro mingi ya ardhi hususani Wilaya za Kilindi, Handeni pamoja na baadhi ya maeneo katika Wilaya zingine, kama Ccm Mkoa wa Tanga lengo letu ni kushirikiana na serikali kuangalia namna bora na nzuri ya kutatua migogoro hii ama kuipunguza kwa kiasi kikubwa" amesema.


"Sisi kama viongozi tulioaminiwa na kupewa dhamana hatuna sababu ya kumsubiria hadi Rais, Makamu au Waziri mkuu wafuke kuja kutatua migogoro yetu, tutampa kazi kubwa sana lakini pia ni aibu kubwa sana kwetu sisi, hatuwezi kukubali"


Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa chama pia kina lengo la kujiimarisha kisiasa na kiuchumi kwani ni vigumu kufanya siasa kama chama hakina vyanzo vya mapato vinavyojitosheleza kutokana na ukubwa wake, hivyo ni lazima kukaa na kubuni mbinu mpya ya kuongeza vyanzo.


"Sasa ili kuweza kupata fedha ni lazima tuweze kuimarisha vyanzo vya mapato katika Mkoa wetu, mimi sitarajii etu tukae tusubiri wahisani kuleta fedha katika chama, ni lazima tuumize vichwa chama hiki ni kikubwa hatuwezi kutolea macho chanzo kimoja ambacho maingizo yake ni ya msimu" amesisitiza.


"Hivyo basi tunahitaji kusimamia vyanzo vilivyopo lakini pia kutafuta vyanzo vingine vikubwa, nitakaa na viongozi wenzangu na kamati ya siasa tuumize vichwa tuangalie ni kwa namna gani tutapata vyanzo vingine vikubwa ambavyo vitatuingizia mapato na kuimarisha chama chetu" amesema.


Hata hivyo amesisitiza kuwepo kwa heshima kwenye katiba, kanuni na miongozo ya chama na jumuiya zake.

Post a Comment

0 Comments