Ticker

6/recent/ticker-posts

CHADEMA KUFANYA MKUTANO WAKE KWANZA WA HADHARA JANUARI 21


Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Kanda ya Victoria, Zacharia Obad akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maandalizi ya mkutano unaotarajiwa kufanyika January 21 kwenye uwanja wa Furahisha uliopo Wilayani Ilemela mkoani Mwanza.


Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakimsikiliza Katibu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kanda ya victoria Zacharia Obad.


*******************


Na Sheila Katikula, Mwanza


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kufanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara January 21 kwenye uwanja wa Furahisha uliyopo wilayani Ilemela mkoani Mwanza baada ya kuruhusiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mikutano hiyo baada ya kufungiwa kwa miaka saba bila kufanyika kwa mikutano ya kisiasa.


Hayo yamesemwa leo na Katibu wa chama hicho wa Kanda ya Ziwa Victoria, Zacharia Obad alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maandalizi ya mkutano huo.


“Tunashukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuzingatia misingi ya sheria na kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara hivyo tunaomba watanzania wafike kwa wingi kutusikiliza kwani tumehakikishiwa ulinzi wa kutosha”, amesema Obad. 


Amesema Chadema kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuheshimu katiba inayotoa haki ya kufanyika kwa mikutano ya kisiasa.


Amesema kufanyika kwa mikutano hiyo kutasababisha kukuwa kwa uchumi kwa kuwa hoteli,vyombo vya usafiri,nyumba za wageni na mama lishe watatoa huduma kwa wageni watakaofika kwenye mikutano hiyo.


Mkutano huo utahudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho ngazi ya taifa.

Post a Comment

0 Comments