Ticker

6/recent/ticker-posts

EQUITY BANK YAANZA MWAKA 2023 KWA KUZINDUA KAMPENI "TUMERAHISISHA"


Watumishi wa Equity Bank Tanzania wakionesha mabango yenye jumbe mbalimbali ambazo zimerahisishwa ili mteja aweze kupata huduma nafuu kupitia benki hiyo leo katika uzinduzi rasmi wa kampeni ya "TUMERAHISISHA" ambapo mteja wa Equity Bank wanaweza kupata huduma za kibenki kirahisi zaidi hasa katika kukuza uchumi na kuboresha maisha.Uzinduzi huo umefanyika leo Januari 17,2023 Jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania Bi.Isabella Maganga akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya "TUMERAHISISHA" ambapo mteja wa Equity Bank wanaweza kupata huduma za kibenki kirahisi zaidi hasa katika kukuza uchumi na kuboresha maisha.Uzinduzi huo umefanyika leo Januari 17,2023 Jijini Dar es Salaam




**********************

BENKI ya Equity Tanzania imezindua rasmi kampeni ya "TUMERAHISISHA" ambapo mteja wa Equity Bank wanaweza kupata huduma za kibenki kirahisi zaidi hasa katika kukuza uchumi na kuboresha maisha.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Januari 17,2023 Jijini Dar es Salaam wakati akizindua kampeni hiyo , Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania Bi.Isabella Maganga amesema kwa mwaka 2023 wao kama wafanyakazi wa benki ya Equity wamejipanga kuhakikisha wateja wao wanaendelea kupata huduma bora za kifedha kwa kupitia hasa teknolojia.

"Tumeanda na kuitambulisha rasmi kauli mbiu yetu ya mwaka 2023 ambayo inakwenda kwa jina la "TUMERAHISISHA", huduma zetu tumezifanya kuwa na gharama za nafuu zaidi, tumelenga kila mtanzania aweze kupata huduma za kibenki, huduma za kibenki zisiwe mzigo kwa watanzania na tumefanya hivyo kwa maana kwamba tunataka kila mtanzania wawe wateja wa benki ya Equity". Amesema

Amesema katika kampeni hiyo pia wamerahishsia katika kujali muda kuhakikisha kwamba huduma zao zinapatikana kwa muda muafaka hususani kwenye huduma za mikopo kwani imekuwa ni changamoto kwa wafanyakazi na wafanyabiashara.

Katika kutoa huduma wamehakikisha kwamba mahusiano na taaluma wanaweka mbele zaidi kuhakikisha kwamba wanawashauri wateja wao vizuri kwahiyo matawi ya yote nchini wapo maofisa maalumu ambao wapo kwaajili ya kuhudumia na kushauri wateja wetu na kutoa ushauri wa kitaalamu utamsaidia mteja katika kufikia malengo yake.

Aidha Bi. Isabella amesema katika huduma wamerahisha katika kufungua akaunti ambapo utaipata hapo hapo na kupewa kadi yako pamoja na kuunganishwa kidigitali kwenye simu yako, pia wamerahisha kuweza kupata huduma kupitia kwa mawakala wao nchini kwa kuweka na kutoa fedha kwa urahisi.

Post a Comment

0 Comments