Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE YA SHERIA NDOGO YAPOKEA TAARIFA YA WIZARA YA UTAMADUNI


*******************

Na Shamimu Nyaki

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo imepokea taarifa ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu hoja mbalimbali za uchambuzi kuhusu Kanuni ziitwazo Licensing and Rights To Benefit From Re- Sale, Regulations ambazo zimeanzishwa na Sheria ya HakiMiliki na Hakishiriki.

Akiwasilisha Taarifa hiyo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul amesema, wizara imefanyia kazi hoja mbalimbali ilizoagiza na Bunge katika vikao vya Kamati vya mwezi Aprili 2022.

"Wizara imepokea Hoja 06, kutoka katika Kamati na imezifanyia kazi kupitia Ofisi ya Hakimili na Hakishiriki ( COSOTA) ikiwemo kuzifuta baadhi ya Kanuni na kutengeneza nyingine ambazo zipo Ofisi ya mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuhakikiwa na kupewa kibali" amesema Mhe.Gekul.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Dkt. Jasson Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijini ameelekeza wizara kukamilisha mchakato wa kutengeneza Kanuni hizo, mapema na kuziwalisha kwa Kamati hiyo kwa ajili ya hatua zinazofuata.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Said Yakubu, Afisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA Bi. Doreen Sinare na Viongozi wengine wa Wizara.

Post a Comment

0 Comments