Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMISHNA TFS PROF. SILAYO ATETA NA WADAU WA UHIFADHI MIKOKO NCHINI


Na Mwandishi Wetu,

Dar es Salaam.

Kamishna wa Uhifadhi – TFS Prof. Dos Santos Silayo amefanya mazungumzo mkurugenzi wa Asasi isiyo ya Kiserikali PLAN VIVO Ms Fiona ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili umuhimu wa kushirikisha jamii na wenyeji katika uhifadhi wa bahari na pwani katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kupunguza utegemezi wa mazao ya mikoko.

Ambapo katika mazungumzo hayo Kamishna wa Uhifadhi ameihakikishia taasisi hiyo ya PLAN VIVO kuwa milango ipo wazi muda wote na huku akiwaahidi kuwapa ushirikiano wakutosha katika kuhakikisha mikoko na pwani inahifadhiwa.

“Nikuhakikishie kwamba TFS itashirikia na asasi yako bega kwa bega kuimarisha usimamizi wa mikoko, na leo nakukabidhi kwa Mratibu wa Misitu ya Mikoko nchini Tanzania, Mhifadhi Mkuu Frank Sima ili muanze utekelezaji mara moja wa yale mliopanga kufanya kwa ajili ya kuhifadhi mikoko lakini pwani pia,” anasema.

Akizungumza kuhusu ujio wake Ms Fiona aliyekuwa ameambatana na Diwani wa Kata ya Mchafukoge wilayani Ilala, Dar es Salaam Mh Mariam Lulida alisema anakusudia kushirikiana na TFS katika Usimamizi wa Hifadhi za Mikoko kupitia uanzishwaji wa shughuli mbadala za Wanajamii kujiongezea kipato Ili kupunguza utegemezi wa mazao ya mikoko.

Alizitaja shughuli hizo kuwa ni pamoja na unenepeshaji wa Samaki aina ya Kaa na Kilimo Cha mwani.


Post a Comment

0 Comments