Ticker

6/recent/ticker-posts

KANOUTE AIPELEKA SIMBA SC 16 BORA ASFC


TIMU ya Simba SC imetinga hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuichapa bao 1-0 Coastal Union kutoka jijini Tanga mchezo uliopigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba SC walipata bao kupitia kwa kiungo wao mkabaji Saido Kanoute dakika ya 56 baada ya kuachia shuti kali lililoenda moja kwa moja na kumshinda mlinda mlango wa Coastal Union.

Mechi nyingine African Sports ya Tanga imesonga mbele kwa ushindi wa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 na New Dundee Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma na Mbeya City imeitupa nje Mbeya Kwanza kwa kuichapa 1-0 Uwanja wa Maji Maji mjini Songea.

Singida Big Stars imeitupa nje Ruvu Shooting kwa kuichapa 2-1 Uwanja wa LITI mjini Singida, Geita Gold imeitoa Nzega United kwa kuichapa 1-0 Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.

Timu ya KMC nayo imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Copco FC ya Mwanza mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments