Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiweka Jiwe la Msingi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliopo iliopo eneo la Mwawaza kata ya Negezi katika Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 18 Januari 2023. Viongozi wengine ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel , Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yahaya Nawanda wakati akikagua maendeleo ya Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika hospitali hiyo leo tarehe 18 Januari 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimpa pole mtoto aliefika kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wakati Makamu wa Rais akiweka jiwe la msingi katika hospitali hiyo leo tarehe 18 Januari 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikagua vifaa tiba vilivyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika hospitali hiyo leo tarehe 18 Januari 2023.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akifurahi pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi na Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi mara baada ya kuweka jiwe la msingi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 18 Januari 2023.

*********************************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 18 Januari 2023 ameweka Jiwe la Msingi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliopo iliopo eneo la Mwawaza kata ya Negezi katika Manispaa ya Shinyanga iliogharimu shilingi bilioni 9.5 mpaka sasa.

Akihutubia viongozi,watumishi wa hospitali pamoja na wananchi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga waliojitokeza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amesema ujenzi wa hospitali hiyo ni mwendelezo wa dhamira ya Serikali kuboresha na kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi. Ameongeza kwamba kuwekwa kwa vifaa tiba kama vile CT- Scan katika Hospitali hiyo kuna lengo la kupunguza adha ya kusafiiri kwenda katika hospitali za mbali kama vile Bugando na Muhimbili ili kupata huduma hiyo. Makamu wa Rais ametoa rai kwa uongozi wa Wizara ya Afya, Mkoa wa Shinyanga , wataalam, wauguzi pamoja na wananchi wote kwa ujumla kutunza vyema majengo na vifaa tiba vilivyopo hospitalini hapo.

Makamu wa Rais amesema serikali itapeleka shilingi bilioni sita katika hospitali hiyo ili iweze kukamilisha ujenzi wa jengo maabara pamoja na jengo la Mama na Mtoto. Vilivile serikali inatarajia kuanza ujenzi wa barabara ya kilometa tano kuingia hospitalini hapo kwa kiwango cha lami ambapo tayari shilingi Bilioni saba zimetolewa.

Halikadhalika Makamu wa Rais ameiagiza TAKUKURU kuweka mkazo katika vituo vya kutolea huduma za afya kuhakikisha watumishi wanaowadai wananchi rushwa wanashughulikiwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria. Pia ameagiza vyombo vya dola kufuatilia na kuwabaini watu wote wanaofanya wizi wa dawa katika Mahospitali na Vituo vya Afya. Vilevile amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuhakikisha Madirisha ya Wazee katika hospitali yanafanya kazi na pia kuhakikisha huduma za dawa kwa wazee zinatolewa ipasavyo.

Pia Makamu wa Rais ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya kifua kikuu na kutumia dawa kwa usahihi kwa wale wenye maambukizi. Amiagiza Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na Wizara ya Afya kuhakikisha sheria na kanuni za afya na usalama mahala pa kazi ikiwemo migodini zinafuatwa. Pia amewaasa kuendelea kutoa elimu kwa wamiliki wa migodi na wachimbaji kuhusu namna bora ya kujikinga na vumbi wanapokuwa katika shughuli za uchimbaji wa madini kwa sababu vumbi la migodini ni kichocheo kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa huo wa kifua kikuu.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Mkoa wa Shinyanga umeokoa jumla ya shilingi milioni 403 katika kusafirisha wagonjwa kwa mwaka baada ya kuwekwa kwa vifaa tiba vya kisasa katika hospitali ya rufaa ya mkoa huo ikiwemo X- Ray pamoja na CT-Scan.

Post a Comment

0 Comments