Ticker

6/recent/ticker-posts

MWAKA 2023 VIJANA WASHAURIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI



*************************

NA MAGRETHY KATENGU

Ikiwa Leo Dunia inasherekea mwaka mpya 2023 Vijana wote nchini wameshauriwa kuanza mwaka kwa kishindo kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwemo kuomba mkopo katika halmashauri zao ili waweze kujikwamua kuchumi.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es saalam na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji,umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Ilala Mohamed Balhabou wakati wa ziara yao ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kata ya Vingunguti iliyopo wilayani Ilala Vingunguti Dar es salaam ikiwemo mradi wa machinjio ya Vingunguti eneo la mabucha ya kisasa na kuhifadhia pamoja na kukatia nyama,daraja la juu katika mradi wa SGR pamoja na Zahanati ya Vingunguti na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa waliolazwa katika zahanati hiyo, pia kushuhudia bonanza la michezo.

"Mimi na vijana wa Chama cha mapinduzi wa kata ya Vingunguti na viongozi wao,Bw Balhabou tumefanya usafi kwa kusafisha maeneo mbalimbali ya hospitali hii na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo sabuni ya kuogea na kufulia ya watoto pamoja na taulo za watoto wachanga (pamprers) kwa akina mama waliojifungua katika zahanati hiyo hii ni Moja ya kuonesha kuwa tunajali"amesema Mohamed

Sanjari na hayo amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kuhakikisha wanaomba mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa vikundi mbalimbali ili iwasaidie kufanya shughuli zao za kiuchumi badala ya kulalamika hali ngumu ya kimaisha.

"Nimeshazungumza na vijana kuhusu asilimia 10 za halmashauri ambayo kati yake vijana hupewa asilimia 4 ya mikopo hiyo,kinamama asilimia 4 na walemavu asilimia 2 kwa hiyo nimewahamasisha waichangamkie kwani haina riba hivyo wakachukue kwa vikundi vyao kwa ajili ya kujiendeleza"amesema Mohamed

Kuhusu miradi aliyoitembelea amesema wao kama vijana wameridhishwa na jinsi miradi hiyo inavyotekelezwa kupitia ilani ya chama cha mapinduzi CCM,ambayo pia imetoa fursa za ajira kwa vijana wa kata hiyo ikiwemo mama lishe kubeba zege na kuwahakikishia kuwa atazifikisha changamoto za vijana Sehemu sahihi ili zitatuliwe.

Naye mwenyekiti wa umoja wa vijana kata ya Vingunguti Mikidadi Kyando amesema hatua ya kufanya usafi katika zahanati na kuwasaidia wagonjwa katika wodi ya wazazi,zahanati ya Vingunguti ni kuwafanya vijana wawe na moyo wa kujitolea kufanya kufanya kazi za kijamii katika maeneo mbalimbali ya umma na hatua ya kutoa misaada ni sehemu ya kumsemea Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan Kwa juhudi anazofanya katika kuleta maendeleo huku akiwataka wananchi kuwapuuza wapinga maendeleo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wenyeviti wa serikali za MITAA kata ya Vingunguti Sharifu Abdala Mbulu ambaye pia ni mwenyeti wa serikali ya mtaa wa Vingunguti amesema Vijana wengi hupenda michezo hivyo weandaa bo bonanza la mchezo wa Mpira wa miguu ili kuwakusanya vijana pamoja na kuibua vipaji kupitia michezo kwani hii ipo kwenye ilani ya CCM .

Post a Comment

0 Comments