Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT.HUSSEIN MWINYI AFUNGUA DIKO NA SOKO LA SAMAKI MALINDI UNGUJA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe.Yusushi Misawa, akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 10-1-2023 na (kushoto) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Spaka wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kulifungua Jengi Jipya la Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja leo 10-1-2023, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Mkewe wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Balozi wa Japan Nchi Tanzania Mhe. Yusushi Misawa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Waziri wa Uchumi wa Buluu Zanzibar Mhe. Suleiman Masoud Makame.(Picha na Ikulu)

MUONEKANO wa Jengo Jipya la Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja lililofunguliwa leo 10-1-2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni kuadhimisha sherehe za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika mnada wa Samaki katika Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja leo 10-1-2023, akinadiwa Samaki aina ya Jodari na Dalali wa Soko hilo Bwa. Ali Hassan Mchoro, samaki huyo amebarikiwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi kwa shilingi 95,000/ katika mnada huo na (kushoto kwa Rais) Balozi wa Japan Nchini Tanzania Mhe. Yusushi Misawa, Waziri wa Uchumi wa Buluu Zanzibar Mhe. Suleiman Masoud Makame, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zana Ahmed Said.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akinunua Samaki katika Diko na Soko la Samaki Malindi Unguja Wilaya ya Mjini leo 10-1-2023, kwa mchuuzi Bwa. Khamis Hamad Omar, baada ya kufunguliwa Soko hili na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni Shamrashamra za Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WASANII wa Kikundi cha Ocean Art cha Mwanakwerekwe Unguja wakitowa burudani ya igizo la Uchumi wa Buluu wakati wa ufunguzi wa Diko na Soko la Samaki Malindizi Wilaya ya Mjini Unguja leo 10-1-2023.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalumu na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrissa Mustafa Kitwana, wakati wa Ufunguzi wa Diko na Soko la Samaki Malindi Wilaya ya Mjini Unguja leo 10-1-2023, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments