Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUTEKELEZA MIRADI 12 YENYE GHARAMA YA SH.113 BILIONI KWA MWAKA 2022/2023 KUPITIA MSCL


Afisa Uhusiano wa Kampuni ya huduma za Meli(MSCL) Edmond Rutajama akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Erick Hamis kwenye kikao kazi kilicho wakutanisha Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mkoani Mwanza.
Baadhi ya Waandishi wa vyombo mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya huduma za Meli(MSCL)


************Na SHEILA KATIKULA,MWANZA

Serikali inatarajia kutekeleza miradi 12 itakayo gharimu kiasi cha sh Bilioni 113 kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023 kupitia kampuni ya huduma za Meli nchini(MSCL)

Hayo ameyasema leo na Afisa Uhusiano wa kampuni ya huduma za Meli (MSCL) Edmond Rutajama wakati akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo,Erick Hamis kwenye

kikao kazi kilicho wakutanisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mkoani Mwanza.

Amesema miradi Saba itagharimu kiasi cha Sh, Bilioni 53 itakuwa katika ziwa Tanganyika na miradi mitano itagharimu kiasi cha Sh Bilioni 57 itakuwa Mkoani Mwanza na sh Bilioni 2 zitatumika kuendesha meli walizopewa na Mamlaka ya Bandari.

"Fedha hizo zitagawanywa katika miradi minne ambayo ni Mipya na miradi mitano ambayo ni ya ukarabati na mingine mitatu inayoendelea kutekelezwa na MSCL ikiwemo, Ujenzi wa Meli ya Mv Mwanza hapa Kazi tu inayojengwa.

Rutajama amesema meli ya Mv Mwanza hapa kazi tu itagharimu kiasi cha Bilioni 108 mpaka kukamilika ambapo mpaka hivi sasa imefika asilimia 80 tangu ilipoanza kutengenezwa.

"Mv Mwanza Hapa kazi tu ni meli kubwa kuliko Meli zote za ukanda wa maziwa makuu, kwani imetuheshimisha wananchi na serikali kwa ujumla "amesema Rutajama.

Post a Comment

0 Comments