Ticker

6/recent/ticker-posts

SHAMRA SHAMRA BURUDANI WIKI YA SANAA TUKITANE DAR FEBRUAR 1-5


 Mtendaji Mkuu wa BASATA Kedmon Mapana (katikati) akizungumza nq waandishi  wa habari  leo  Januari 31,2023. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Nafasi Art Space Lilian Mushi na kulia kwake  Mkurugenzi Mstaafu wa Naface Arts Space Rebecca Corey

*********************

Na Magrethy Katengu

Baraza la Sanaa la Taifa ( BASATA) Kwa kushirikiana na taasisi ya Nafasi Arts Space wamejipanga kuhakikisha kutoa burudani kwa Watanzania katika wiki ya Sanaa huku kazi za wasanii zikisambazwa kila kona na kujipatia kipato kupitia vipaji vyao.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Nafasi Art Space Lilian Mushi wakati akitoa taarifa juu ya Maadhimisho ya kufanya toleo la pili la wiki ya Sanaa lijulikanalo kama"Tukutane Dar" linalotarajiwa kufanyika kuanzia Februari 1 hadi 5 mwaka huu ikiambatana na matukio mbalimbali ikiwemo Warsha,mijadala ya hadhara,maonyesho ya Sanaa ikiwakutanisha wataalamu na wadau wa Sanaa ndani na nje ya nchi kwa kuwaleta kujenga mfumo mahiri na mtandao wa Sanaa na utamaduni

"Kwa kuzingatia mafanikio ya toleo la kwanza la mwaka 2020 Tukutane Dar kwa mwaka 2023 ikifanyika katika maeneo saba ya Sanaa na kitamaduni kote Jijini Dar es salaam ikijumuisha Maeneo ya Nafasi Arts Space,Rangi Gallery ,CDEA ,Ajabu Ajabu ,ASEDEVA,Chuo Kikuu cha Dar es salaam na MuDa Kona,sehemu hizi zitaandaa majadiliano ya paneli asubuhi na warsha na maonyesho ya wasanii jioni" amesema Liliani.

Hata hivyo Mkurugenzi Lilian Warsha hizo zitajumuisha Darasa la Utunzaji kazi za Sanaa litakaloendeshwa na watunzaji wa Sanaa wa Kimataifa,kutakuwepo na warsha ya Uandishi wa filamu,warsha ya "Threatre" Kwa maendeleo ya Jamii, na warsha ya kuchora ramani za maeneo ya ubunifu kote Tanzania.

Sanjari na hayo amesema Siku ya Ijumaa Februari 3 kutakuwa na wataalamu wa Sanaa kutoka Afrika kusini,Uingereza,Zambia na Uganda,watafanya mjadala wa hadhara katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam( UDSM) ,ambapo siku ya Jumamosi ya Februari 4 Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA Dkt Kedmon Mapana ,Katibu Mtendaji wa BASATA wataelezea sera mpya ya Baraza hilo na namna wasanii Wanaweza kunufaika na sera hizo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa BASATA Kedmon Mapana amesema serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa BASATA imekuwa ikiweka mazingira mazuri kuwawezesha wasanii kwa kuwapatia mikopo isiyo ya riba ili waweza kukuza na kuendeleza vipaji vya Sanaa Ili kufikia malengo wanayotamani kufika.

"Taasisi ya Arts Space ni Muhimu sana kwenye kuibua vipaji na kuviendeleza,imeandaa tukio hili kubwa kwa ajili ya kukutana wadau wa Sanaa nakujadili Kwa pamoja changamoto na mafanikio ya Sanaa,lengo ni kukuza tasnia ya Sanaa hapa nchini" amebainisha Dkt Mapana.

Pia Dkt Mapana amesema kupitia wiki hiyo siku ya tarehe 3 mwaka huu kutakuwa na kuleta mrejesho wa kileta mchakato uliokuwa ukifanyika mdundo wa Taifa na vazi la Taifa

Nae Mkurugenzi Mstaafu wa Naface Arts Space Rebecca Corey amesema kwamba taasisi hiyo imefanikiwa kushirikiana vizuri na serikali nakwamba itaendelea kushirikiana na wadau wengine wa Sanaa katika kuibua,kukuza na kuendeleza kazi za wasanii mbalimbali hapa nchini.

Hata hivyo Nafasi Arts Space imewaomba wapenzi wote wa Sanaa na utamaduni kushiriki na kuungana kwa pamoja na wasanii na wataalamu wa sanaa kutoka ndani na nje ya Tanzania ,pamoja na kufurahia shughuli za kitamaduni zitakazo fanyika kuzunguka Jiji la Dar es salaam na kutambua maeneo mengine Tanzania yanayojihusisha na shughuli za Sanaa na utamaduni kupitia wawakilishi wa Mikoa.

"Ratiba kamili ya matukio inaweza kupatikana kupitia mitandao ya Kijamii ya Nafasi Art Space na tovuti na kurasa za mitandao ya Kijamii za washirika wenzetu" imesema taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Nafasi Arts Space Lilian Mushi.

Post a Comment

0 Comments