Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZANIA YAMPOKEA SPIKA WA BUNGE LA WANANCHI KUTOKA NCHINI INDIA

Spika wa Bunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Spika wa Bunge la Wananchi wa India Mr Om Birla wakifanya mazungumzo katika Ofisi ndogo za Bunge leo Januari 18,2023 Jijini Dar es Salaam
Spika wa Bunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Spika akipokea zawadi kutoka kwa Spika wa Bunge la Wananchi nchini India Mr Om Birla katika Ofisi ndogo za Bunge leo Januari 18,2023 Jijini Dar es salaam

Spika wa Bunge Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Spika wa Bunge la Wananchi nchini India Mr Om Birla wakipeana mikono katika Ofisi ndogo za Bunge leo Januari 18,2023 Jijini Dar es Salaam

**************************

Na Magrethy Katengu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amepokea ugeni kutoka nchini india ambaye ni spika wa Bunge la Wananchi wa India Mr Om Birla na baadhi ya wabunge kuja kuangalia fursa zilizopo nchini Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za bunge zilizopo Jijini Dar es salaam Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson amesema ujio wa ugeni huo ni wa kihistoria kwani tokea miaka hamsini iliyopita ndio taifa liliwahi kupata ugeni kama huo.

"Tumezungumza mambo mengi mojawapo ya mambo ambayo tumezungumza nao ni ushirikiano wa kibunge kati ya bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,baraza la wawakilishi Zanzibar pamoja na bunge la wananchi wa India, tumezungumza kuamsha mahusiano yetu ya mihumili hii miwili lakini pia kutumia chuo chao cha mafunzo ambapo mafunzo hayo yanatolewa kwaajili ya wabunge na watumishi wa bunge" Alisema Dkt Tulia.

Ameongeza kuwa nchi zetu zimekuwa na mashirikiano yanayoendelea kudumu katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya,maji,kilimo,Elimu, na sekta ya teknolojia ambapo madaktari wa Tanzania na India wamekuwa wakibadilishana uzoefu na kupata mbinu mpya za kitabibu na upasuaji.

Kwa upande wake spika wa bunge la wananchi nchini India Mr Om Birla amesema india Wapo tayari kuendeleza maradufu mahusiano mazuri ya kibunge yaliyoanza tangu miaka mingi kwani kupitia mashirikiano hayo imesaidia kuibua fursa mbalimbali za kiuchi

Ameongeza kuwa India na Tanzania zimeendelea kuwa mashirikiani mazuri ya kinchi katika sekta mbalimbali tokea mwaka 1961 ambapo india ndio ilianzisha ubalozi wake nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments