Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI WA CCM KUANZIA NGAZI YA SHINA WASHAURIWA KUSHIRIKIANA KUTATUA KERO ZA WANANCHI


Na Magrethy Katengu

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde amewashauri Viongozi wa Jimbo la Ukonga kuanzia ngazi ya Shina ikiwemo balozi wenyeviti katibu wenezi kata kufanya kazi kwa ushirikiano katika kutatua kero za wananchi iwasaidie kujiwekea imani kwa wapiga kura wao kuelekea Uchaguzi 2024 -2025

Wito huo ameutoa Jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Chama Cha CCM uliofanyika Ukonga na kukutanisha Viongozi kutoka kata mbalimbali za Jimbo hilo kuanzia ngazi ya Shina ambapo amewasisitiza kila mmoja kutimiza wajibu wake ipasavyo kwa moyo wa ujasiri na kujitolea kwani kufanya hivyo ni kulisaidia Taifa kupiga hatua ya kimaindeleo .

"Mimi naongea hivi ila sijui wewe kiongozi ugumu unaopitia katika kata yako kwani dhamana uliyopewa kuwatumikia wananchi ni vyema wajumbe wa chama hiki mkashirikiana msimuachie kiongozi mmoja atatue kero za watu kwani kidole kimoja hakivunji chawa mshirikiana huu ni muda muafaka kwa ajili ya maandalizi 2025 Uchaguzi Mkuu CCM ni imara ila kero za wananchi zitatuliwe "amesema.

Katibu amesema CCM viongozi waache kujifungia ndani kusubiria mpaka Uchaguzi ufike wanachama na viongozi watoke nje katika shida na raha za wananchi kwani ikiwa ni desturi yenu hata kampeni zenu zitakuwa hatutatumia nguvu sana wananchi wanachotaka kuona ni utendaji siyo maneno .

"Hatukosi changamoto katika mitaa yetu tuwe na lugha na kauli Moja katika mikutano yetu ya hadhara tusikosoane mbele ya wanachi mengine ya ndani tunamalizana katika vikao vyetu vya ndani nawasihii zingatieni maelekezo yote yaliyotolewa ni muda wa ..

Aidha ametoa wito kwa viongozi wote kuwa Kadi za CCM zipo tayari wao wanatakiwa kuanza harakati za kuongeza wanachama wapya kwani kuna vijana ambao ni chipukizi wamefikia umri wa kupata kadi na bado hawajapata





Post a Comment

0 Comments