Ticker

6/recent/ticker-posts

VIPENGELE VYA SHERIA INAYOMLINDA MTUHUMIWA WA UKATILI KUONDOLEWA.




************************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


SERIKALI imesema iko tayari kurekebisha au kufuta kabisa baadhi ya vipengele vya sheria ambavyo vinawalinda wahalifu wanaofanya makosa ya ukatili wa kijinsia ili kuwapa amani wananchi kwa kutoa hukumu kwa wahalifu hao.

Hivyo kukitaka Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake nchini (TAWJA) kuainisha vipengele wanavyoona vinamlinda mtuhumiwa kuachiwa huru na kosa limethibitishwa, vipelekwe bungeni ili viangaliwe namna ya kutenda haki ipatikane.


Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge Dr. Tulia Akson kabla ya kuzindua mkutano mkuu wa 11 wa majaji na mahakimu wanawake nchini (TAWJA) uliofanyika jijini Tanga ambapo amesema wananchi wanatakiwa kujiridhisha na hukumu ya wahalifu Ili kuwaondolea maswali.


Dr. Akson amebainisha kwamba kwa kawaida wananchi wanapomkamata muhalifu ambaye amefanya kitendo cha ukatili wanampeleka polis wakijua atapata hukumu lakini baadae anaachiwa huru na kusababisha maswali na masononeko kwa walliomkamata.


"Mimi niseme Bunge liko tayari kabisa, kama sheria zinaleta changamoto, hawa wanaoitwa watuhumiwa baadaye wanaachiwa huru kulingana na sheria yetu ilivyo, tuko tayari kubadilisha ili watu wote wawe salama lakini pia kila mtu awe na amani, kwa sababu amani hata ya mtu binafsi inakuwepo anapoona anatendewa haki".


Aidha ameitaka TAWJA kutoa elimu kwa wananchi juu ya sheria katika kufanya maamuzi yao na utoaji haki kwani watapoelimishwa na kuelewa hawatakuwa na mashaka kwenye maamuzi yanayotolewa na katika mahakama kulingana na makosa ya mtuhumiwa.


"Ili jamii yetu iweze kuelewa utaratibu wa utoaji haki ni lazima update elimu, na kwa sababu ninyi TAWJA mmejipambanua kama chama cha utoaji haki ambao mnapambania usawa wa kijinsia, lakini pia mnapogana dhidi ya ukatili unaotokea kwa wanawake, watoto na watu wenye ulemavu,


"Kwahiyo kwenye eneo hilo elimu ikitolewa watu wakafahamu mipaka yenu ya maamuzi, sasa hapo ni lazima mtumie sheria na siyo kuona na kusema unatoa maamuzi, hapo utakuwa hujantumia sheria" amebainisha.


Kwa upande wake Jaji mkuu wa mahakama nchini Profesa Ibrahim Juma amebainisha kwamba TAWJA wanatekeleza salamu za Rais Samia Sulluhu Hassan ambazo alitoa siku ya mwaka mpya 2023 kwamba watahakikisha wanafanyakazi za utoaji haduma katika haki kuliko miaka mingine iliyopita.


Profesa Juma amesema TAWJA pamoja na mahakama kazi zai kubwa ni utoaji haki na kuelimisha umma katika maeneo ya utoaji wa haki za binadamu, kujenga uwezeshaji miongoni mwa wadau wa haki za binadamu, upatikanaji wa haki ya Yale makundi yaliyopo katika hali hatarishi, wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.


"Sisi mahakama tunajivunua sana uwepo wa hiki chama cha TAWJA, muhimili wa mahakama unakichukulia kama chombo maalumu ambacho kinaleta taswira na muonekano kwamba mahakama ni taasisi inayojali usawa wa kijinsia na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia" amesema.


"Pia kimetusaifia sana kuondoa taswira ya mfumo dume na tunapofanya kazi zetu wananchi wanaojua kweli mahakama zinatenda haki, lakini pia niwapongeze sana kwa kazi zao nyingi za kujitolea kwa wananchi" ameeleza.


Mwenyekiti wa TAWJA Joaquina De- Mello amefafanua kwamba chama hicho kilianzishwa mwaka 200 kama chama cha kijamii na dhima nzima ya ikiwa ni haki sawa kwa wote kwa kuzingatia utawala wa sheria na usawa wa kijinsia.

Post a Comment

0 Comments