Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAFUNZI WA KIDATU CHA NNE NA SITA KUKABIDHIWA ZAWADI ZAO ZA KOMPUTA (LAPTOP) NA RAIS DKT. HUSSEIN MWINYI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Kishikwambi Afisa Mdhamani Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Bwa.Mohammed Nassor, kwa ajili ya matumizi ya Walimu wa Skuli za Msingi na Sekondari Pemba,(kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Leila Mohammed Mussa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Tanzania Mhe. Prof.Adolf Mkenda,wakati wa hafdla ya kukabidhiwa Komputa (Laptop)kwa Wanafunzi wa Kidatu cha Sita na cha Nne waliofanya vizuri Mitihani yao kwa mwaka 2022, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-1-2023.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, akimkabidhi zawadi ya Komputa(Laptop) Mwanafunzi wa Kidatu cha Sita Skuli ya Sekondari Lumumba Mohammed Faki Hamad, kwa kufanya vizuri Mitihani yake ya Taifa mwaka 2022 na kupata Daraja la kwanza, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-1-2023.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi Komputa Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Tumekuja Kidatu cha Nne Zakia Jaffar Hatib, kwa kufaulu Mtihani wake wa Taifa Kidatu cha Nne na kupata Daraja la kwanza.hafla hiyto iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu leo 11-01-2023.(Picha na Ikulu) WAGENI waalikwa na Wakuu wa Idara za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakihudhuria hafla ya kukabidhiwa zawadi za Komputa (Laptop) kwa Wanafunzi wa Kidatu cha Sita na cha Nne waliofanya vizuri Mitihanin yao ya Taifa mwaka 2022 na kupata Daraja la Kwanza, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-1-2023.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi ya Komputa (Laptop) Mwanafunzi Msabaha Shaban Kassim wa Skuli ya Sekondari ya Lumumba, kwa kufanya vizuri Mitihani wa Taifa ya Kidatu cha Nne mwaka 2022 na kupata daraja la Kwanza, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-1-2023.(Picha na Ikulu)RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali waliokaa na waliosomama ni Wanafunzi Bora waliofanya vizuri Mitihani yao ya Kidatu cha Nne na Sita kwa mwaka 2022, baada ya kukabidhiwa zawadi zao Komputa (Laptop) alizowaahidi hafla hiyo iliyofanyika leo 11-1-2023 katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa kukabidhi zawadi za Komputa (Laptop) alizowaahidi Wanafunzi wa Kidatu cha Sita na Cha Nne waliofanya vizuri mitihani yao ya Taifa mwaka 2022 na kupata Daraja la Kwanza, hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar leo 11-1-2023.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments