Ticker

6/recent/ticker-posts

ACT WAZALENDO WAIOMBA OFISI YA WAZIRI MKUU KUFUATILIA FIDIA ZA WAATHIRIKA MLIPUKO MABOMU MBAGALA 2009***********************

Na Magreyhy Katengu

Chama Cha ACT Wazalendo kimeomba Ofisi ya Waziri Mkuu kulifuatilia sakata la malipo ya Waathirika wa Mabomu ya Mbagala na kuchukua hatua za uwajibikaji kwa watendaji  kwani kuna harufu za Udanganyifu,Ubaguzi na Uonevu.

Rai hiyo imetolewa Februari 1 2023 Jijini Dar es salaam na Waziri Mkuu Kivuli wa Chama hicho Dorothy Semu ambapo amesema watu takribani 1361 wanadai fidia zao tangu 2009 baada ya kuripuka Mabomu kwenye ghala la silaha katika kambi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania( JWTZ) namba 671 KJ iliyopo Mbagala Jijini Dar es salaam.

Amesema kwamba Mripuko huo umesababisha vifo,majeruhi,kuharibiwa kwa makazi na mali za watu pamoja na athari za kiafya ikiwemo magonjwa ya kifua kikuu,upofu wa macho na saratani,ambapo amebainisha kuwa wastani wa kaya 12000 ziliathiriwa na milipuko hiyo katika eneo la Mbagala pekee.

"Januari 28 2023 nilitembelea Mbagala Kufuatilia suala hili baada ya kupokea malalamiko kutoka Kwa Waathirika hao,nilifanikiwa Kufuatilia na kuchambua taarifa mbalimbali ikiwemo orodha ya Waathirika,malipo,risiti za malipo,kiasi Cha bajeti kilichotumika na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) na baadae kutembelea baadhi ya Waathirika hao"amesema

Nakuongeza kwamba "Act Wazalendo tumeshangazwa sana kuona kwa zaidi ya Miaka 14 tangu kutokea kwa milipuko hiyo kuna Waathirika wapatao 1361 kutolipwa fidia yao.

Amesema kuwa malalamiko ya Waathirika hao yapo katika maeneo mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa malipo kiduchu,utaratibu mbovu wa tahmini ya athari za mabomu,Utaratibu wa Malipo kutoeleweka,Wapo waliolipwa miezi kadhaa baada ya bajeti pamoja Usiri wa Malipo hayo.

Aidha amesema kuwa Malalamiko mengi ya wananchi yanathibitishwa na ripoti ya CAG 2012/13 ilionyesha malipo ya fidia Kwa Waathirika wa mabomu ya Mbagala kulipwa kiasi Cha shilingi Bilioni 8 hayakuwa na nyaraka muhimu za kuthibitisha kama kweli malipo hayo yalifanyika kwa walengwa,kinyume chake adhabu hiyo wanapewa wananchi Kwa kunyimwa stahiki zao,Vitisho na kebehi.

Amesema kuwa jambo linaloumiza zaidi ni kuona viongozi wa serikali kuanzia Halmashauri ya Temeke,ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Mambo ya Ndani kutumia vitisho kushughulikia suala hilo kwa kutaka kuzima vilio vya wananchi,ambapo chama hicho kimesikitishwa na kitendo kinachofanywa na serikali cha kushindwa kuwangalia Waathirika hao licha ya Bunge kuidhinisha bajeti ya shilingi Bilioni 17 nakwamba zimekwishatolewa kwa awamu takribani sita.

Hata hivyo amewataka Watumishi wa serikali kusikiliza madai ya wananchi na kutoa ufafanuzi stahiki nakwamba hatua stahiki zichukuliwe Kwa wahusika wa kitengo Cha maafa wanaotoa vitisho kuwapotezea,kuondoa uhai,kuwaapisha kinyume cha sheria,kuwajeruhi kama jitihada za kuwanyamazisha viongozi wa wahanga waliopunjwa fidia ili kuwavunja Moyo wanapodai haki zao.

Post a Comment

0 Comments