Ticker

6/recent/ticker-posts

B.KHADIJA AIPONGEZA ZECO KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA CCM.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Ndg.Khadija Ali Salum,akiwa amembeba Mtoto Riziki Abdalla anayetibiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja aliyetupwa na Mzazi wake baada ya kuzaliwa.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Ndg.Khadija Ali Salum,akizungumza katika eneo linalofungwa Transifoma katika mradi wa ujenzi wa soko la Mwanakwerekwe.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Ndg.Khadija Ali Salum,akiwa katika eneo linapofungwa Transifoma katika mradi wa ujenzi wa soko la Chuini Zanzibar.

MSHAURI muelekezi wa Kampuni ya ujenzi ya Emirates Construtions LTD, Mhandisi Arafa Haji Ali akizungumza na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar (SUKI) Ndg.Khadija Ali Salum,alipokuwa akikagua ujenzi wa Soko la Chuini.

*****************************

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Ndg.Khadija Ali Salum,amelipongeza Shirika la umeme Zanzibar kwa kutekeleza kwa kutekeleza kwa ufanisi maagizo ya Chama Cha Mapinduzi.

Alisema hatua ya Shirika hilo kufunga Transifoma mbili katika maeneo ya miradi ya ujenzi wa masoko inayosimamiwa na Serikali ya awamu ya nane ni ya kupongezwa.

Pongezi hizo alizitoa wakati alienda kuthibisha zoezi la ufungaji transifoma hizo huko Mwanakwere na Chuini, alisema matarajio ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili wananchi wafanye biashara katika mazingira mazuri.

“Ufungaji wa transifoma hizi ni miongoni mwa utekelezaji wa maelekezo na maagizo ya Chama katika kuhakikisha miradi hiyo ya ujenzi wa masoko inakamilika kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa”, alisema Khadija.

Zoezi hilo la ufungaji wa transifoma linatokana na ziara ya kushutukiza ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Mohammed aliyoifanya februari 6,mwaka 2023 ambapo alielezwa kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa nishati ya umeme inayosababisha kushindwa kutumika kwa baadhi ya vifaa vinavyohitaji kiwango kikubwa cha umeme.

Kupitia ziara hiyo Naibu huyo aliagiza shirika la umeme Zanzibar (ZECO) kutatua changamoto hiyo ili kampuni zinazojenga masoko hayo zikamilishe kazi kwa wakati uliopangwa.

Akizungumza Fundi Mkuu wa Shirika hilo Ndg.Omar Yussuf Omar, alisema baada ya kukamilika kwa zoezi la kufunga transifoma hizo watakuwa wamemaliza tatizo la upungufu wa umeme katika miradi hiyo.

Alisema katika eneo la Chuini wamefunga Transifoma yenye ukubwa wa KVA 100/KV 33 na katika mradi wa Mwanakwerekwe wamefunga yenye ukubwa wa KVA 200/KV 11 zenye uwezo wa kuzalisha umeme unaoendana na mahitaji ya ujenzi huo.

“Tunafunga transifoma hizi ambazo ni mpya zitamaliza changamoto ya upungufu wa huduma ya nishati ya umeme katika maeneo ya miradi hii ya ujenzi wa masoko.

Kwa upande wa msimamizi Mkuu wa mradi wa ujenzi wa soko na kituo cha Mabasi katika eneo la Chuini Mhandisi Shamte Ali Shamte, aliipongeza CCM kwa kusimamia zoezi hilo na likatekelezwa kwa haraka.

Mhandisi Shamte, alisema wanatajia kumaliza ujenzi huo Novemba 16, mwaka 2023.

Wakati huo huo , Katibu wa SUKI Ndg.Khadija alitembelea Wagonjwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja na kumkagua mtoto mchanga aliyetupwa na mzazi wake mara tu baada ya kuzaliwa.

Post a Comment

0 Comments