Ticker

6/recent/ticker-posts

KUMBUKUMBU YA MIAKA 44 IMAM KHOMEINI



Miaka 44 iliyopita katika siku kama ya leo; Imam Khomeini (M.A) Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alirejeanchini Iran na kulakiwa na umati mkubwa wa wananchi, baada ya kuwa uhamishoni kwa zaidi ya miaka 10; siku ambayo imebakia kuwa moja ya siku za kihistoria zenyekukumbukwa mno katika historia ya Mapinduzi yaKiislamu ya Iran. 

Kwa hakika Tarehe 12 Bahman 1357 iliyosadifiana na Februari Mosi, 1979 Miladia, ilikuwanukta kuu katika mapambano ya wananchi wa Iran dhidiya utawala wa Shah; na katika kipindi cha siku kumi tutangu kurejea nchini Imam Khomeini, Mapinduzi yaKiislamu yalipata ushindi licha ya uungaji mkono waMarekani kwa utawala wa Shah. 

Baada ya Mfalme Shah kibaraka wa madola ya Magharibikukimbia nchi hapo tarehe 26 Dei 1357 Hijiria Shamsiasawa na tarehe 16 Januari 1979, Imam Khomeini alitangaza uamuzi wake wa kurejea nchini. Uamuzi huowa kishujaa na wa hatari pia uliwatia wasi wasi mkubwawapenzi na wapinzani wa mtukufu huyo. 

Wananchi waIran na licha ya kwamba walikuwa wamefanya subira yamuda mrefu ya kumgonjea kiongozi wao huyo, pia walikuwa na wasi wasi kwamba vibaraka wa utawala wakitwaghuti watamsababishia madhara katika safari yakehiyo ya kurejea nchini. 

Kwa upande mwingine nao utawalawa Shah na waungaji mkono wake wa Kimarekani naWamagharibi walikuwa wanajua kwamba, kurejea Imam Khomeini nchini Iran kutazidisha moto wa harakati za kimapinduzi na hatimaye kufikiwa ushindi wa Mapinduzihayo ya Kiislamu. Baada ya Imam kuazimia kurejeanchini, kulianza harakati nyingi za kuzuia safari yake hiyoya kihistoria. Mkabala wake wanamapinduzi miongonimwa wananchi walitumia uwezo wao wote kwa ajili yakuzishinda njama hizo za maadui ili kufanikisha kiongoziwao huyo anawasili nchini salama salimini.

Wananchi walioshikamana na dini wa Iran walikuwapamoja na Imam Khomeini baada ya kuitikia mwito wake wa kuchukia dhulma. 

Wananchi wa Iran walikuwawameona kuwa, Imam Khomeini alikuwa mtu safi, arif naaliyekuwa akiguswa mno na mambo ya wananchi nahakuwa akifanya hayo kwa ajili ya hawaa na matamaniobali alikuwa kama Imam Hussein AS ambaye alitoka nakuanzisha harakati kwa ajili ya kuhuisha dini na thamaniza Uislamu.

Ni kwa msingi huo ndio maana wananchi waIran wakaitikia mwito wake, na kusimama naye bega kwabega kukabiliana na dhulma na ukndamizaji wa utawalawa mfalme Shah.

Imam Khomeini kama walivyokuwa mababu zakewatoharifu, alikuwa katika harakati na mkondo wa kuleawatu na jamii na katika sentesi moja tunaweza kusemakuwa, alikuwa akifuatilia suala la kueneza maadili mema.



Kueneza maadili na tabia njema ni miongoni mwa amri za Mwenyezi Mungu katika Qur’ani kwa Nabii wake MtukufuMuhammad SAW, ili wale wote wanaotaka kuingia katikaUislamu wafahamu kwamba, utawala na siasa sio mambo ambayo yako kando na utukufu wa mwanadamu namasuala ya kimaanawi; bali jamii bora ya Kiislamu itafikiadaraja hiyo kwa kufungamana tu na masuala haya mawilimuhimu. Mwenyezi Mungu SWT anawakumbushaWaislamu kuhusiana na hili katika Aya ya 21 ya Surat al-Ah’za kwa kusema:

Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume waMwenyezi Mungu kwa anayemtaraji Mwenyezi Mungu naSiku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungusana.

Kwa hakika Mtume SAW alikuwa ruwaza njema ya juukabisa ya mtawala wa Kiislamu na baada yake, Imam Ali bin Abi Twalib (as) ambaye alichoroa na kudhihirishaumbo la uadilifu wa kijamii na utukufu wa mwanadamukatika kipindi cha utawala wake wa Kiislamu.

Imam Khomeni pia akifuata nyayo za shakhsia wakubwawa kidini, alikuwa katika mkondo wa kuhuisha na kuenezathamani za kidini katika jamii. Jamii ambayo itajengwakatika misingi ya Uislamu na fikihi ya Kishia na hivyo, tabia njema, maadili mema, bila shaka masuala ya kimaanawihujitokeza na kudhihirika bayana katika jamii hiyo.

Hapana shaka kuwa, utawala kama huu ulikuwa ukihitajiakiongozi ambaye yeye mwenyewe amebobea katikataaluma ya fikihi, mwenye utambuzi sahihi na mpana wadini, aliyejipamba kwa taqwa na uchaji Mungu na maadilimema; ambapo Imam Khomeini alikuwa na sifa zote hiziaali.

Mwanzoni mwa ujana wake, Imam Khomeini alijishuhulisha na kulea nafsi yake na kujibidiisha katikakujiimarisha zaidi katika maadili mema na sifa njema. Kwa hakika shakhsia huyo hakuwa na mithili katika kuchungamaadili na kushikamana na taqwa na kumuogopaMwenyezi Mungu.

Walioishi chumba kimoja na Imam Khomeini wakati akiwa masomoni walikuwa wakifahamukwamba, Ruhullah Khomeini ana sifa kuu mbili: Sifa yakwanza ni kuamka usiku wa manane kwa ajili ya kuswaliSwala ya Suna ya usiku. Sifa ya pili ni kujiweka mbalikabisa na kusengenya watu, bali hata kusikiliza watuwakisengenya.

Shakhsia wa namna hii alikuwa akitilia mkazo mno sualala kusema kweli na kutenda mema, na inawezekanakusema kuwa, ‘ukweli katika kauli na matendo’ ni vigezoambavyo viliwavutia zaidi watu katika shaksia ya Imam Khomeini (Rahmatullah Aleih)


Kusema kweli tupu na kujiepusha na uongo ni katikamaamrisho ya Mwenyezi katika Qur’ani pamoja namiongozo ya viongozi wa dini na wakati huo huo nimiongoni mwa ishara za imani, taqwa na uchaji Mungu. Imam Ali AS anasema: Kusema kweli ni nguzo imarakabisa ya dini.

Imam Khomeini alikuwa mtiifu kwa kile alichokuwaakikisema iwe ni katika maisha yake binafsi au maishayake ya kisiasa. Alipokuwa akiwanasihi maafisa waserikali na suala la kutoikumbatia dunia na kuishi maishaya kawaida yasiyo na ufakhari, basi yeye alikuwa kigezocha kweli kabisa katika hayo. 

Wakati wananchi wa Iran walipoona tamu ya ukweli katika maneno na vitendo vyaImam Khomeini (Quddisa Sirruh) walimuamini na kuwapamoja naye zaidi katika njia yake ya Mapinduzi na nikatika mazingira haya ndipo wananchi Waislamu wa Iran wakawa tayari kufa shahidi katika njia ya kumtetea nakumhami kiongozi wao huyu.

Imam Khomeini alikuwa Marjaa mkubwa wa kidini na arifna wakati huo huo mwanasiasa mahiri, mwenye upeo wahali ya juu, aliyekuwa na shakhsia ya kuvutia na yenyeushawishi kwa watu, aliyekuwa dhidi ya udikteta naambaye hakuwa na utegemezi siyo kwa madola makubwaya Magharibi wala ya Mashariki. 

Kwa upande wa busurina muono wa mbali sambamba na mtazamo wa kina kuhusiana na masuala ya jamii alikuwa na upeo na ustadiwa aina yake katika zama zake, kama ambavyo alikuwamweledi wa masuala ya mataifa mengine ya dunia.

Aidha Imam Khomeini alifahamika kwa kuwa mtu waratiba, mipango, unadhifu na utanashati, na moja ya siri za mafanikio yake ni kwamba, alikuwa na mipangomadhubuti ya kielimu na kivitendo, katika uongozi na hatakatika harakati zake za kisiasa.


Historia inaonyesha kuwa, alikuwa akiandaa jedwali na ratiba kwa ajili ya kazianazopaswa kufanya mathalani kesho.

Aidha jedwali hilolilikuwa limejaa kazi na shughuli katika masaa yote isipokuwa nyakati za usiku ambapo alikuwa akiamka nakuswai Swala ya usiku na kunong’ona na Mola wake.

Imam Khomeini alikuwa na mipango maalumu na makinikiasi kwamba, watu waliokuwa wakimzunguka kwakumuona Imam Khomeini akifanya jambo fulani basiwaliweza kujua hivi sasa ni saa ngapi. 

Hii ni kutokana nakuwa, Imam Ruhullah Khomeini alikuwa na wakatimaalumu wa kula chakula, alikuwa na wakati maalumu wakulala na alikuwa akiamka katika saa na wakati maalumu. Hata anapokuwa na miadi na mtu alikuwa akifika kwawakati bila kuchelewa hata kidogo.

Sayyida Zahra Mustafavi, binti wa Imam Khomeini anasimulia kwa kusema:

Imam alikuwa makini na mtu wa wakati kiasi kwamba, ikitokea amechelewa dakika chache tu kwa ajili yachakula, watu wake wa nyumbani walikuwa wakiingiwa nawasiwasi.

Hivyo wote bila ya kupenda hujipatawameelekea katika chumba ya Imam, na wanapofika hukohumkuta kwa mfano Ahmad mtoto wa Imam amewasilihapo na alikuwa akimuuliza maswali baba yake, ambayenaye hakuwa na budi isipokuwa kumjibu na hivyokumfanya achelewe.

Tunakamilisha Makala yetu yaliyojiri kwa manasaba wasiku hizi za kumbukumbu ya Alfajiri Kumi kuelekea kilelecha maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa kunukuu maneno ya Ayatullah Ali Khamenei, KiongoziMuadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambaye ni mmojawa wanafunzi wa Imam Khomeini.

Ayatullah Khamenei anasema: Imam Khomeini alikuwa katika rehema nafadhila za Mwenyezi Mungu kutokana na kuwa kwake namahusiano na mafungano na Mwenyezi Mungu. 

Hebu, njooni na sisi tuendeleze njia yake kwa kumtegemeaMwenyezi Mungu, kuwa na ikhlasi na nia njema (katikaamali na matendo yetu) na kufanya hima, idili na kuwa naazma na msimamo thabiti.

Aliyekutayarishia na kukuletea Makala hii ni mimi SalumBendera. Nakutakieni kila la kheri. Kwaherini.

Post a Comment

0 Comments