Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA RAIS WA ZIMBABWE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Makamu wa Rais Zimbabwe ambaye pia ni Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mheshimiwa Generali ( Mstaafu) Constantino Chiwenga,Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 01 Februari 2023.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja Makamu wa Rais Zimbabwe ambaye pia ni Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mheshimiwa Generali (Mstaafu) Constantino Chiwenga mara baada ya Mazungumzo yao yaliofanyika Jijini Dar es salaam leo tarehe 01 Februari 2023.

*************************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 01 Februari 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais Zimbabwe ambaye pia ni Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mheshimiwa Generali (Mstaafu) Constantino Chiwenga,Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema Tanzania inathamini urafiki wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili ambao umekuwepo tangu enzi za harakati za Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.

Amesema Tanzania itaendelea kudumisha na kukuza zaidi ushirikiano uliopo pamoja na kuungana na nchi hiyo kupinga vikwazo mbalimbali vinavyoikabili.

Makamu wa Rais amesema Tanzania inaunga mkono Ujenzi wa Makumbusho ya Historia ya Ukombozi wa Afrika inayojengwa Mjini Harare Zimbabwe na inaipongeza sana Zimbabwe kwa kuamua kuandika na kuhifadhi historia muhimu ya vuguvugu la Ukombozi hususani kusini mwa Afrika.

Dkt. Mpango amesema Tanzania inalenga kuendelea kukuza ushirikiano wa kibiashara na Zimbabwe pamoja na sekta za kilimo, utalii, uwekezaji, kukuza lugha ya Kiswahili pamoja na elimu ya juu.

Kwa Upande wake Makamu wa Rais Zimbabwe Mheshimiwa Generali (Mstaafu) Constantino Chiwenga amesema Tanzania ni nchi ambayo imetoa mchango mkubwa kwa Zimbabwe na nchi za Kusini Mwa Afrika katika harakati za ukombozi ambao kamwe hautosahaulika.

Amesema kwa sasa mataifa haya yanapaswa kujielekeza zaidi katika ushirikianio wa kiuchumi kwa kuwafanya wananchi wake kutumia fursa ya ushirikiano uliopo kukuza uchumi wao na kujiletea maendeleo na kurithisha ushirikiano huo vizazi na vizazi.

Generali (Mstaafu) Constantino Chiwenga amesema kwa sasa Zimbabwe inaednelea na Ujenzi wa Barabara kutoka Harare kupitia Zambia ambayo inalenga kupunguza zaidi ya kilometa 300 katika kuifikia bandari ya Dar es salaam hiyo hakuna budi kuongeza ushirikiano katika sekta za madini, mawasiliano, kilimo, sekta ya fedha, ulinzi na usalama.

Aidha ameishukuru Tanzania kwa kuungana nan chi hiyo katika kupinga vikwazo vya kiuchumi pamoja na kuiunga mkono katika ujenzi wa Makumbusho ya Historia ya Ukombozi wa Afrika Jijini Harare.

Pia Chiwenga amesema inapaswa mataifa haya mawili kutumia vema fursa za uwekezaji zilizopo katika nchi hizo pamoja na fursa ya Ukanda Huru wa Kibiashara Barani Afrika kwa kujiletea maendeleo.

Post a Comment

0 Comments