Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC HOI KIMATAIFA, YACHAPWA 3-0 NA RAJA CASABLANCA*************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imeshindwa kupata pointi kwenye mechi yake ya pili hatua ya makundi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo imepokea kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Raja Casablanca ya nchini Morroco.

Katika mchezo huo ambao Simba Sc alikuwa mwenyeji ambapo mechi ilichezwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, Raja Casablanca walifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 30 kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Hamza Kabba.

Bao la pili la Raja Casablanca limefungwa na Soufiane Benjdida dakika 83 ya mchezo baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kufanikiwa kuweka kambani.

Raja Casablanca walipata bao la tatu kwa mkwaju wa penati kupitia kwa beki wao Ismail Mokadem

Hii ni mechi ya pili Simba Sc haijaambulia chochote kwenye michuano hiyo kwani mechi ya kwanza waliookea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Horoya.

Post a Comment

0 Comments