Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WAOMBWA KUJITOKEZA CCM KIRUMBA FEBRUARI 8 KUSIKILIZA NENO LA MUNGU

Askofu wa jimbo la kaskazini wa kanisa la waadventista sabato (SDA) Marck Malekana akizungumza na Waandishi wa habari mkoani hapa kuhusu ziara ya Rais wa kanisa hilo,Teddy Wilson ambaye anatoka Maryland nchini Marekani.


*************************

Na Sheila Katikula, Mwanza

Waumini wa madhehebu mbalimbali wameombwa kujitokeza kwa wingi Februari 8 mwaka huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba ili waweze kusikiliza neno la mungu litakalo tolewa na Rais wa kanisa la Waadventista Sabato (SDA),Teddy Wilson ambaye anatoka Maryland nchini Marekani.

Hayo yamesemwa leo na Askofu wa jimbo la Kaskazini, Marck Malekana wakati akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mkoani hapa.

Amesema ni vema kila muumini wa madhehebu mbalimbali kutokeza ili aweze kusikiliza neno la mungu.

Amesema lengo la ziara hiyo nchini Tanzania ni kuzungimza na waumini juu ya neno la mungu h sanjari na kuangalia maendeleo ya kanisa hilo.

" Wilson atawasili mkoani hapa Februari 8 saa tano asubuhi na kufanya misa na mahubiri kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Amesema Rais huyo ambaye ametoka kutoka makao makuu ya SDA ,Maryland nchini Marekani atatembelea mataifa matatu yakiwemo , Tanzania , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Kenya.

"Rais atatembelea na kutoa wakfu kwa ajili ya huduma zinazofanyika katika hospitali ya Pasiansi ambayo imeanza kutoa huduma za matibabu ya kibingwa katika manispaa ya Ilemela.

Post a Comment

0 Comments