Ticker

6/recent/ticker-posts

KINANA AKUTANA NA MABALOZI WA MAREKANI NA MISRI, WAZUNGUMZIA KUIMARISHA UHUSIANO

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini Michael battle, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo. (Picha na Fahadi Siraji /CCM)

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akimsindikiza Balozi wa Marekani hapa nchini Michael battle, mara baada ya mazungumzo yao leo Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam,.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Misri nchini Tanzania Sherif Abdelhamid Ismail (kushoto) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na Balozi wa Misri nchini Tanzania Sherif Abdelhamid Ismail (kushoto) pamoja na Ujumbe alioambatana nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam. (Picha Zote na Fahadi Siraji /CCM)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akipokea zawadi kwa Balozi wa Misri nchini Tanzania Sherif Abdelhamid Ismail (kushoto) katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam.

*********************


Leo Machi 14, 2023

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amekutana na kufanya Mazungumzo na, Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Michael Battle, katika Mazungumzo yao Wamegusia Kuimarisha Ushirikiano. 

Kwa upande wa Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Mhe. Michael Battel ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa Namna inavyoendelea kupiga hatua katika kuimarisha Demokrasia, Utawala wa Sheria, Uhuru wa Kisiasa na Utawala bora. 

Aidha Ndg Abdulrahman Kinana amekutana na Kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri Nchini Tanzania Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail ambapo pamoja na mambo mengine, Balozi huyo ameahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali mbali ikiwa pamoja na kuimarisha biashara na uwekezaji kwa ajili ya kunufaisha pande zote.

Post a Comment

0 Comments