Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Gerald Msabila Kusaya kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ally Senga Gugu kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Aretas James Lyimo kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.

Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro Tixon Tuyangine Nzunda, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Gerald Msabila Kusaya, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Ally Senga Gugu, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Aretas James Lyimo pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) wakila Kiapo cha Maadili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Tamisemi Anjellah Kairuki, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka pamoja na Makatibu Tawala walioapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 19 Machi, 2023.

Post a Comment

0 Comments