Ticker

6/recent/ticker-posts

TAKUKURU TANGA YAJA NA PROGRAMU RAFIKI.********************


Na Hamida Kamchalla, TANGA.


TAASISI ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Tanga imezindua programs mpya ya 'TAKUKURU Rafiki' itakayoongeza ushiriki wa kila mwananchi katika kukabiliana na tatizo la rushwa.

Kaimu mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga Victor Swella ameyasema hayo kwa waandishi wa habari, kwamba programs hiyo pia itasaidia katika utoaji wa huduma kwa jamii pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.


Swella amebainidha kwamba utekelezaji wake ni kuwa na vikao katika ngazi ya kata ili kutambua kero zilizopo katika utoaji na upokeaji wa huduma kama za afya na elimu, ambazo zikiachwa pasipo kutatuliwa zitapelekea vitendo vya rushwa, pamoja na mchakato wa kutelekeza miradi ya maendeleo.


"Baada ya kutambua kero hizo, washiriki wa vikao hivyo wakiwemo wananchi, viongozi wa serikali, kisiasa na wazabuni, watashirikiana kutatua kero zilizopo au kuweka mikakati ya jinsi ya kuzitatua kwa pamoja" amesema.


"TAKUKURU itaeatibu uendeshaji wa vikao hivyo na utekelezaji wa mikakati itakayowekwa, ikiwemo kutoa mrejeaho kwa umma juu ya kero zitakazoibuliwa na kutatuliwa ili kufikia malengo ya programu hii" amebainisha Swella.


Aidha ametoa wito kwa kila mwananchi anapaswa kushiriki katika kufichua vitendo vya rushwa kwa kutoa taarifa kwa TAKUKURU ili kwa pamoja kuweza kuimarisha udhiniti wa rushwa.


Pia amefafanua kwamba TAKUKURU imejipanga na itaendelea na uzuiaji wa rushwa katika ukudanyaji wa mapato ya serikali kwa niia ya kielektroniki (POS) ili kuweka udhiniti madhubuti kwa lengo la kuongeza ufanisi katika ukudanyaji wa mapato.


"Tutajielekeza pia kwenye ufuatiliaji wa miradi ya ujenzi katika Wilaya zote za Mkoa wa Tanga ili kuhakikisha kwamba fedha zinazotolewa na serikali zinatumika ipasavyo kumaliza miradi husika kwa wakati na ubora unaolingana na fedha halidi" amesema.


"Kwa hili, ninawakumbusha wasimamizi wa miradi ya maendeleo kuzingatia uadilifu na uaminifu katika utekelezaji wa majukumu yao, popote walipo, TAKUKURU ipo, hatutasita kuchukua hatua stahili dhidi ya wale wote watakaofuja fedha zilizotolewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo" amebainisha.


Hata hivyo Swella amebainisha kwamba katika kipindi cha octoba hadi disemba mwaka 2022, wakifuatilia miradi ya ujenzi katika Wilaya ya Korogwe ambapo walibaini kulikuwepo na hasara iliyotokana na ukiukwaji wa kanuni na taratibu kwa upande wa manunuzi.


Miongoni mwa miradi waliyofuatilia ni pamoja na ujenzi wa vyumba 11 vya madarasa katika shule za sekondari Semkiwa, Kimweri na Nyerere ambayo ilitengewa jumla ya sh milioni 220 kutoka serikali kuu, sambamba na mwongizo wa kutumia mfumo wa manunuzi wa fedha za ndani.


"Ufuatiliaji huo umezuia hasara ya sh milioni 17 ambazo serikali ingepata sababu ya ukiukwaji wa taratibu katika manunuzi ya bidhaa za ujenzi wa miradi husika, kwa sasa madarasa yote yanaendelea kutumiwa na wanafunzi wapya waliojiunga na kidato cha kwanza mwaka huu " ameeleza.

Post a Comment

0 Comments