Ticker

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA ASILIMIA 90 WAKAZI WANAOISHI BONDE LA MSIMBAZI WAMESHAFANYIWA UTHAMINI WA MALI ZAO

Mratibu Miradi ya Serikali inayotekelezwa na na Mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia Mhandisi Humphrey Kanyenye.

***************

Na Magrethy Katengu

Zaidi ya asilimia 90 ya Wakazi waishio eneo la Bonde la Mto Msimbazi wameshafanyiwa uthamini wa viwango wanavyotakiwa kufidiwa ili kupisha Mradi wa daraja lenye urefu Kilometa 390 litakalosaidia eneo athari za Mafuriko lisiathirike hususani barabara

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mratibu Miradi ya Serikali inayotekelezwa na na Mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia Mhandisi Humphrey Kanyenye amesema hatua ya hii ya kutolea ufafanuzi ni baada ya kusikia baadhi ya Wakazi wanaoishi katika eneo la bonde la Msimbazi kulalamika kuhusu ulipwaji wa fidia.

Hata hivyo amesema katika eneo hilo kutokana na Mfululizo wa changamoto ya Mafuriko kuanzia mwaka 2011 hadi 2018 zaidi ya Wakazi 3400 waliokuwa wakiishi hapo serikali ililazimika kuwahamishia kuishi Mabwepande hivyo kwakua serikali inathamini wananchi wake licha eneo hilo kutolewa nots ya kuwa eneo hilo ni hatarishi Kwa kuishi lakini waliendelea kuendeleza makazi yao kwa kujenga na kupanda miti.

"Serikali yetu ni sikivu inatambua hali za wananchi wake hivyo kikao cha kwanza kilitishwa mwaka 2018 Januari na Rais Dkt Samia Suluhu Hassani wakati akiwa Makamu wa Rais aliunda timu kuangalia namna bora ya kuwalipa fidia Wakazi wanaoishi eneo hilo kwa kufanya uthamini na sehemu ya Mali zitakazoathirika Mradi huo ikiwemo nyumba miti na kujua viwango namna ya kulipa"amesema Mhandisi

Sanjari na hayo amesema Zoezi la kuwathamini wakazi 258 Wakazi wameshafanyiwa na zoezi linaendelea na wataletewa fomu ya kujaza kufanyiwa uhakiki kisha watajaza kukubalina na viwango kila mmoja anavyohitajika kufidiwa.

Aidha kulingana na eneo hilo lilishatolewa nots kuwa ni eneo hatarishi kuishi tangu mwaka 1979 ulipaji fidia hautahusika kulipa ardhi isipokuwa kile kilichokuwa juu ya ardhi ikiwemo gharama ya nyumba na miti iliyopandwa hivyo wakazi hao kwa kwa kuwa walishapewa Elimu walio wengi ambao tayari wameshafanyiwa uthamini wekubaliana na zoezi linaendelea Kwa wengine .

Post a Comment

0 Comments