Ticker

6/recent/ticker-posts

GAVU AHIMIZA KUSOMESHA WATOTO ELIMU YA DINI KUWAJENGA KATIKA MAADILI MEMA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Oganaizesheni, Issa Gavu amesema kuwa kuwekeza katika elimu ya dini kwa vijana ni kuwajengea nyezo muhimu ya kimaadili isiyofutika katika maisha yao.

Gavu ameyasema hayo leo Aprili 9, 2023 aliposhiriki mashidano ya Qur’an wilayani Mafia, Mkoa wa Pwani.

Akizungumza katika mashindano hayo yaliyondaliwa na Mbunge wa Mafia ambaye pia ni Naibu wa Waziri wa Elimu, Sanyasi na Teknolojia, Omari Kipanga, Gavu alisema ni muhimu kwa wazazi kuwasimamia watoto kujifunza elimu ya dini.

Kwa mujibu wa Gavu mbali ya kuwajengea uwelewa wa kiimani, lakiniu pia kusomesha watoto elimu dini kuandaa kizazi chenye maadili mema na kumtambua Mwenyezi Mungu.

“Hivyo wakati wazazi wakiendelea kuwekeza elimu ya jumla kwa watoto, wasisiahau kuwekeza pia kwenye elimu ya dini kwani ndio inayowajenga zaidi vijana kiimani na imani hudumu zaidi katika nyoyo za watu,” alisema.

Hafla hiyo ya mashindano ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mafia.


Post a Comment

0 Comments