Ticker

6/recent/ticker-posts

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE MWAKA 2023 AMPONGEZA MFANYABIASHARA SUPERFEO KWA UWEKEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim,akiweka mafuta kama ishara ya ufunguzi rasmi wa kituo cha mafuta cha HM Petrol Station kinachomilikiwa na mfanyabiashara Omari Msigwa(Superfeo) kulia, kilichagarimu zaidi ya Sh.bilion
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaibu Kaim,akikata utepe kufungua rasmi kituo cha mafuta cha HM Petrol Station kinachomilikiwa na mfanyabiashara maarufu hapa nchini Omari Msigwa(Superfeo.

Mmiliki wa kituo cha mafuta cha HM Petrol Station Omari Msigwa(Superfeo) wa pili kulia,akimuongoza Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaibu Kaim wa pili kushoto kwenda kufungua kituo hicho eneo la Osterbay Msamala Manispaa ya Songea,kushoto meneja wa kituo cha HM Lucas Komeka.

Kituo cha mafuta cha HM Petrol Station kinachomilikiwa na mfanyabiasahara maarufu wa kampuni ya Superfeo Omari Msigwa.


******************

Na Muhidin Amri, Songea

SERIKALI imempongeza mfanyabiashara maarufu nchini Omari Msigwa(Superfeo),kwa kuwekeza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyosaidia kutoa ajira kwa vijana wengi hapa nchini.

Pongezi hizo zimetolewa jana na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaibu Kaim,baada ya kukagua na kuzindua rasmi kituo cha mafuta cha HM Petrol Station, kinachomilikiwa na Superfeo kilichopo eneo la Msamala Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Alisema,hatua ya Msigwa kuwekeza miradi mingi ya kiuchumi hapa nchini imewezesha kuisaidia serikali ya awamu ya sita katika mkakati wake wa kupunguza tatizo la ajira na kukusanya mapato na kodi kutokana na uwekezaji uliofanywa na Superfeo katika mikoa mbalimbali.

Alisema mfanyabiashara huyo amekuwa msaada mkubwa kwa Watanzania,na serikali itahakikisha inampa kila aina ya msaada ili aweze kufanikisha katika shughuli zake na kuwataka wafanyabiashara wengine kuiga mfano wa Superfeo kwa kuwekeza nyumbani badala ya kwenda nje ya nchini.

Mkuu wa wilaya ya Songea Wilman Ndile alisema,Superfeo ni Mtanzania mzalendo aliyeamua kujenga na kuwekeza vitega uchumi nyumbani kutokana na kuwepo kwa mazingira wezeshi ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Alisema,Supefeo ameajiri Watanzania wengi kutoka mikoa mbalimbali na amekuwa mlipa kodi mzuri kutokana na shughuli anazofanya ndani na nje ya mkoa wa Ruvuma.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Superfeo &Selou Tours Omari Msigwa,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kumpa ushirikiano mkubwa katika jitihada zake anazofanya na kutambua mchango wake kwa Watanzania.

Amewaomba watanzania kumuunga mkono kwa kuitumia kampuni hiyo kwa shughuli za usafiri na usafirishaji wa bidhaa pamoja na huduma ya mafuta inayotolewa katika kituo cha HM Petrol Station kilichopo katika eneo la Msamala.

Meneja wa kituo cha mafuta cha HM Petrol Station Lucas Komeka alisema,mradi huo umegharimu kiasi cha Sh.bilioni 1,255,000,000 hadi kukamilika.

Alisema,mradi huo unatoa huduma ya kuuza mafuta aina ya Disel na Petroli,Mgahawa,kuosha na matengezo ya magari,kutoa huduma za fedha kupitia mashine(ATM)duka la bidhaa mbalimbali(Min Super Makert) na kukata tiketi.

Alieleza kuwa,kituo kina uwezo wa kujaza mafuta magari 10 kwa wakati mmoja na kwa siku kina uwezo wa kuhudumia vyombo vya moto 150 na tangu kilipoanza kutoa huduma kimekuwa sehemu ya kuharakisha kukua kwa uchumi wa wilaya ya Songea,mkoa wa Ruvuma na Taifa.

Post a Comment

0 Comments