Ticker

6/recent/ticker-posts

MTATURU APAZA SAUTI BUNGENI.


MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ametaka serikali itoe kauli kuhusu wazee walio zaidi ya miaka 60 kufanya shughuli za vijana ikiwemo kutengeneza barabara na kuchimba mitaro kinyume na sheria.

Akiuliza swali hilo April 5,2023,Jijini Dodoma,Mtaturu amesema zoezi la kukwamua familia maskini kupitia TASAF ni zuri na huko nyuma lilikuwa kwa ajili ya kuwalipa kwenye mambo mbalimbali.

“Mh Spika hivi karibuni kumeongezwa package ya kuwapa kazi wazee halafu wanalipwa,na maeneo mengi tumeanza kuona wazee wetu wakitumikishwa wanafanya kazi zaidi ya miaka 60 kitu ambacho sio kizuri serikali inasemaje?,maana wanafanya kazi ya kutengeneza barabara na kuchimba mitaro kazi ambayo ilikuwa inalenga vijana,”ameuliza.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhwani Kikwete amekiri uwepo wa malalamiko katika baadhi ya maeneo kuhusiana na wazee waliozidi umri wa miaka 70 kufanya kazi ambazo zipo katika mazingira ya kufanya vijana.

Kutokana na hilo amesema tayari serikali imeshatoa mwongozo unaoongoza shughuli za TASAF,kwamba wazee wote walio juu ya miaka 60 na akina mama wajawazito pamoja na watoto wadogo hawaruhusiwi kufanya kazi katika mazingira hayo na ikitokea mzee amelazimishwa basi sheria itafuata mkondo wake katika kuchukua hatua za msingi.

Post a Comment

0 Comments