Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT HUSSEIN MWINYI ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI MEI 3,2023

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Dkt. Rose Reuben (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 6,2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo hufanyika Mei 3 kila mwaka huku Kitaifa yanatarajiwa kufanyika Zanzibari kuanzia Mei 1-3 2023 yakiongozwa na kauli mbiu isemayo"Kuunda Mustakabali wa Haki".

*******************

Na Magrethy Katengu

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo hufanyika Mei 3 kila mwaka huku Kitaifa yanatarajiwa kufanyika Zanzibari kuanzia Mei 1-3 2023 yakiongozwa na kauli mbiu isemayo"Kuunda Mustakabali wa Haki".

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Dkt. Rose Reuben amesema Umoja wa Mataifa uliidhinisha siku hiyo mwaka 1993 ikiwa na lengo la kukuza Uwelewa wa umuhimu wa Uhuru wa Vyombo vya habari kukumbusha serikali na jamii kuheshimu na Uhuru wa habari kama inavyolindwa katika ibara ya 19 ya tamko la Ulimwengu la haki za binadamu

" Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari Duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Mei 3 tangu Umoja wa Mataifa ilipoidhinisha siku hii mwaka 1993 na hapa nchini kama wadau na wanahabari tumeendeleza utaratibu huu kuadhimisha siku hii kila mwaka lengo ni kukuza Uelewa wa umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari na kukumbusha serikali pamoja na jamii kuheshimu na kulinda haki ya uhuru kama inavyolindwa katika ibara ya 19 ya tamko la Ulimwengu la haki za binadamu"amesema Rose

Hata hivyo Dkt Rose amesema mwaka huu maadhimisho hayo yanatimiza miaka 30 hivyo katika mwaka huu katika siku hiyo tukakuwa na siku mbili ya kufanya midahalo mbalimbali ikiwemo kuangalia wapi kuna changamoto na mafanikio yaliyopatikana hivyo wanahabari wote wanaoomba kuwa mstari wa mbele kuhabarisha Umma na kutoa taarifa kwa kuzingatia maadili yanayozingatia tasnia ya habari

Waandishi wa habari hawana budi kuheshimiwa wanapotekeleza Majukumu yao kwa kuwa na Uhuru wa kujieleza pasipo kubugudhiwa wanapotumia haki ya kikatiba kuhabarisha Umma kwani kuna haki ya uhuru wa kujieleza usalama wa wanahabari kwani tunaona Sasa wanahabari uhuru wa kujieleza unazidi kushambuliwa jambo ambalo linaathiri utekelezaji wa haki nyingine za binadamu"amesema Dkt Rose

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya habari Maelezo Rodney Thadeus amesema Serikali inatambua Umuhimu wa vyombo vya habari ndiyo maana kila jambo lazima liwaite Wadau wote wa sekta hiyo Kwa kupokea maoni yao ikiwa kama kuna Mabadiliko ya kisheria Ili waridhie wenyewe kabla haijapelekwa Bungeni kujadiliwa na kupitishwa kuwa sheria

Naye Afisa Habari Kutaifa kituo cha habari Umoja wa Mataifa Ofisi ya Mratibu Mkaazi wa Mashirika ya UN Tanzania Nafisa Didi amesema ni wakati muafaka wa kutafakari jinsi Mabadiliko ya kidigitali na Maendeleo ya kiteknolojia yanayotaka msisitizo mpya wa Uhuru wa kujieleza kama kichocheo kikuu na kiwezeshaji kufurahia haki nyingine zote za binadamu

"UNESCO ni Shirika la Umoja wa Mataifa lenye Mamlaka maalumu ya kukuza uhuru wa kujieleza upatikanaji wa Maendeleo ya habari katika mtandao na nje ya mtandao kama msingi muhimu ya demokrasia na Maendeleo msaada wetu unakusudia kujenga mazingira wezeshi na uwezo wa wabebaji wajibu haki kama sharti la kulinda na kukuza haki nyingine zote za binadamu"amesema Nafisa

Aidha Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake Kwa kushirikiana na Taasisi zaidi ya 20 za kihabari za Kitaifa nchi chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wataungana kuadhimisha Siku hiyo adhimu Kitaifa inatarajiwa kufanyika Zanzibari na Mgeni Rasmi atakuwa Rais Hussen Mwinyi Maadhimisho hayo yataambatana na midahalo kuanzia Mei 1-2 na Mei 3,2023 ndiyo Maadhimisho yenyewe katika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar

Post a Comment

0 Comments