Ticker

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA ISTIQAAM KWA KUSHIRIKIANA NA MSIKITI WA IBAADH WATOA MSAADA KWENYE KITUO CHA SOS.


Na Sheila Katikula Mwanza

Taasisi ya Istiqaam Kwa kushirikiana na msikiti wa Idaadh wametoa msaada katika kituo Cha kulelea watoto Cha SOS kilichopo Mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati akitoa msaada huo Mjumbe wa Taasisi hiyo Rashid Self ameeleza kuwa wameguswa kutoa msaada huo ili na watoto wanaoishi katika kituo hicho waweze kufarijika hususani katika kipindi chiki cha sikukuu ya Idd.

Self ameeleza kuwa Taasisi hiyo utaendelea na kituo hicho began kwa bega kuhakikisha watoto hao wanaendelea kuwa na furaha.

"Watoto wenu ni watoto wetu tutawaangalia Kwa pamoja Kwa kidogo tulichojaliwa na Mwenyezi Mungu," amesema Self.

Sheikh wa msikiti wa Ibaadh Nouh Mousa ameeleza kuwa wanawashukru watu wote ambao wanaendelea kutoa msaada kwani jambo hilo ni la kheri.

" Laiti watu wangekuwa wanajua thawabu zinazopatikana Kwa kuwapa furaha watoto yatima Kwa kuwapa malazi wangepigania jambo hilo ni jambo lenye baraka usipotoa Mungu hawezi kukupa Kwa sababu Mungu anakupa ili uwape watu wanyonge" Amesema Sheikh Mousa.

Mratibu wa kituo cha kulelea watoto SOS Mwanza Antony Mkinga ameeleza kuwa zipo changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika kuwalea watoto hao ikiwa pamoja na swala la Afya na kutokuwa mawataalamu wa kuweza kuwalea watoto wenye mahitaji maalumu.

Mkinga ametoa wito kwa Taasisi na vituo vyote kufata miongozo, Taratibu na kanuni zilizotolewa na serikali kuhakikisha watoto hao hawafanyiwi ukatili wa aina yeyote ile.

Kwa upande wao walezi wa kituo hicho Sheila Mohamed na Mariamu Juma wameeleza kuwa wanaishukru taasisi hiyo Kwa kuwapatia msaada huo.

" Watoto wa hapa wanahitaji faraja kitu kikubwa wanachokikosa ni upendo na faraja wakiona watu kama hawa wanakuja kuwatembelea wanapata faraja sana" walisema.

Aidha wametoa wito Kwa wadau wengine na mashirika mbalimbali kuguswa na kuona watoto wanauhitaji mkubwa na kuendelea kujitolea na kuwasaidia.

Post a Comment

0 Comments