Ticker

6/recent/ticker-posts

TFS, WADAU WA UHIFADHI WAWEKA MIKAKATI KUREJESHA UOTO WA ASILI,WASEMA HEKTA 400,000 ZINAHARIBIWA KILA MWAKA NCHINI

Na Said Mwishehe,

HEKTA zaidi ya 400,000 za ardhi zinaharibiwa kila mwaka nchini kutokana na mambo mbalimbali kubwa ikiwa ni shughuli za kibanadamu,hivyo hatua mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa na wadau wa mazingira ili kunusuru hali hiyo na kurejesha uoto wa asili ulioharibika.

Katika jitihada hizo leo Aprili 27,2023 Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wamewakutanisha wadau mbalimbali wa Misitu, Uhifadhi na mazingira jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili fursa zitakazowezesha kufikia malengo ya kurejesha hekta milioni 5.2 za uoto wa asili ifikapo mwaka 2030 ikiwa ni kutimiza lengo la nchi 32 zilizopo Afrika

Kwa ujumla wake nchi hizo zimejiwekea mikakati ya kutekeleza hatua hiyo , hivyo zinatakiwa kurejesha jumla ya hekta milioni 100 kwa kipindi hicho na kwamba malengo hayo yatakelezwa kwa wadau kuendelea kuweka mipango na kuitekeleza.

Akizungumza kwenye kikao hicho cha wadau, Mhifadhi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) Juma Mwangi ametaja mikakati ambayo Tanzania imejiwekea ni kwamba hadi kufikia mwaka 2030 iwe imetimiza lengo la nchi za Afrika mashariki kurejesha hekta milioni 5.2 za uoto wa asili.

"Lengo hilo litafanikiwa pindi wadau mbalimbali watakapotoa ushirikiano kupitia fursa zilizopo. Shughuli za kilimo cha kuhamahama ,ufugaji na masuala ya ujenzi pamoja na matumizi ya miti kama nishati kwa watanzania waliowengi zimechangia uwepo wa uharibifu wa mazingira,"amesema Mwangi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI) Dkt. Revocates Mushumbusi amesema uharibifu wa mazingira nchini ni mkubwa sana na unaotokana na matumizi ya binadamu ikiwemo kilimo cha kuhamahama, ufugaji, vyanzo vya maji na kushindwa kufuata utaratibu wa mipango miji.

Amesema wadau ambao wamekutana leo pamoja na mambo mengine watajadili malengo ya nchi 32 za Afrika zilizokaa mwaka 2018 na kuweka mipango ya kureejesha hekta milioni 100 za uoto wa asili ifakapo 2030

" Ni utekelezaji wa mkakati wa nchi za Afrika Tanzania ni miongoni nchi zitarejesha hekta milioni tano za uoto wa asili ifikapo mwaka 2030"amesema Dkt. Mushumbusi na kuongeza ahadi kubwa waliyonayo ni kuendelea kutoa elimu kuhusu kurejesha uoto wa asili.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Miradi Kisiki Hai, Njamasi Chiwanga ameeleza taasisi yao lengo ni kukusanya nguvu ili kutimiza malengo hayo."Taasisi yetu zaidi ya asilimia 55 tunafanya kazi hivyo zaidi ya vijiji 400 misitu iko chini yetu na tuna mikakati mingi ya kurejesha ardhi na uoto wa asili."
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)Juma Mwangi akizungumza wakati wa kikoa cha wadau wa uhifadhi, Misitu na Mazingira walipokutana leo Aprili 27,2023 jijini Dar es Salaam kujadili na kuweka mikakati ya kuendelea kurejesha uoto wa asili.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI), Dkt. Revocatus Mushumbusi akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa uhifadhi na mazingira kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi ya Kisiki Hai, Njamasi Chiwanga akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao hicho

Post a Comment

0 Comments