Ticker

6/recent/ticker-posts

UJENZI WA KITUO CHA AFYA SUMVE WILAYANI KWIMBA WAENDELEA
Mkuu wa wilaya ya Kwimba Ng'wilabuzu Ludigija amesema kukamilika Kwa Ujenzi wa kituo Cha afya katika kijiji Cha Sumve Kata Sumve wilayani humo kitawasaidia wakazi wa maeneo hayo kupata matibabu karibu zaidi badala ya kwenda umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

Akiongea wakati wanakijiji na viongozi wa serikali na chama wakishiriki uenzi wa kituo hicho LUDIGIJA amesema mradi huo utachukua miezi minne kukamilika na kwamba Halimashaur ya Kwimba imeshatoa shilingi Milioni 300 na mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF ikitoa shilingi Milioni 136 kuwezesha mradi huo

DC Ludigija amewasihi viongozi na wananchi kuulinda mradi huo kwakuwa unamanufaa makubwa Kwa Wana Sumve na maeneo ya jirani hivyo amekema kitendo Cha baadhi ya watu watakaojaribu kufanya udokozi wa vifaa vya ujenzi au kukwamisha Kwa aina yoyote kuacha mara moja kwakuwa atakumbana na mkono wa sheria

Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashaur ya Wilaya Kwimba amesema shilingi Milioni 300 ni za Ujenzi wa jengo la maabahara OPD na kichomea taka huku TASAF ikitoa Milioni 136 kuwezesha jengo la Wazazi zimetokana na mapato ya ndani na kwamba ndani ya muda wa miezi minne Ujenzi wa kituo hicho utakuwa umekamilika

Wakati huohuo LUDIGIJA amesema serikali imeendelea kupeleka fedha za Ujenzi wa miradi mbalimbali katika Wilaya ya Kwimba ikiwemo Ujenzi wa madarasa na vituo vya afya


Post a Comment

0 Comments