Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI WAHIMIZWA KUDHIBITI, VVU, UKIMWI NA MAGONJWA SUGU YASIYOAMBUKIZA (MSY)


Mkurugenzi wa huduma za Afya Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Rajajbu Mtili, akimkaribisha Mgeni rasmi Prof. Allen Mushi, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha, na Utawala, ili afungue mafunzo ya elimu ya VVU, Ukimwi na MSY.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe mipango, Fedha na Utawala Prof. Allen Mushi akiongea na washiriki wa mafunzo wakati wa ufunguzi wa mafunzo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe mipango, Fedha na Utawala Prof. Allen Mushi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki na Wakufunzi wa mafunzo ya Elimu ya VVU, Ukimwi na MSY.
Mwezeshaji Bi. Juliana Theodori, akitoa mafunzo ya ujumuishwaji wa anuaini za jamii mahali pa kazi
Mwenyekiti wa mafunzo kwa niaba ya washiriki, akitoa neno la shukrani kwa wawezeshaji baada ya mafunzo kukamilika.
Mwezeshaji Dkt. Patrick Kanyamwenye akitoa mafunzo ya VVU, Ukimwi na MSY kwa washiriki.


***************

Waelimisha rika kutoka Chuo Kikuu Mzumbe wamepatiwa mafunzo ya Elimu ya kudhibiti VVU, UKIMWI, na magonjwa sugu yasiyoambukizwa yatakayowawezesha kutoa Elimu hiyo kwa Watumishi na Wanafunzi ili kuhakikisha wanakua na afya bora na nzuri wakati wote wanapokuwa kazini na darasani.

Mafunzo hayo ya siku tatu, yalifunguliwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Allen Mushi, na kuhusisha Waelimishaji Rika kutoka Skuli, Vitivo, Kurugenzi na Vitengo vyote vya Chuo.

Akizindua mafunzo hayo Prof. Mushi, ametoa shukrani kwa kuwepo kwa elimu hii ili kuendana na Sera ya kitaifa juu ya kupambana na magonjwa ikiwa ni kipaumbele cha Taifa namba moja kwa watumishi na Taifa, ikifuatiwa na rushwa.

“Ni wajibu wetu wafanyakazi kupambana na magonjwa ili kuweza kujikwamua na changamoto zinazojitokeza kutokana na magonjwa”. Alisema Prof. Mushi.

Mafunzo haya yamekusudiwa kukuza uelewa wa namna ya kukabiliana na matatizo, pamoja na kuwajengea uwezo waelimishaji na maadili katika kutunza siri za wanaowahudumia, ili kufikia malengo yaliyokusudiwa. Aliongeza Prof. Mushi.

Akitoa mafunzo hayo Bi. Juliana Theodori, Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora aliweka wazi majukumu ya kamati ya VVU, UKIMWI na Magonjwa yasiyoambukiza, na kufafanua sifa za muelimisha rika, na namna shughuli za utoaji elimu zinavyoaswa kufanyika mahali pa kazi.

Naye Dkt. Patrick Kanyemwenye kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TAK-AIDS) alielezea namna watumishi wanavyoweza kudhibiti VVU, Ukimwi na magonjwa yasiyoambikizwa, na tahadhari za msingi za kuchukua katika kujikinga na maradhi. Maeneo mengine yaliyofundishwa kwenye mafunzo hayo ya siku tatu ni pamoja na utofati kati ya VVU na Ukimwi, aina za VVU, upimaji, aina za vipimo na kuhimiza upimaji wa afya kila mara, pamoja na virusi vya homa ya ini.

Mafunzo hayo yalihitimishwa kwa washiriki kupata mafunzo kuhusu elimu ya afya ya akili na changamoto zake, na kuandaa mpango shirikishi juu ya uelimishaji rika sehemu za kazi.

Post a Comment

0 Comments