Ticker

6/recent/ticker-posts

WAMACHINGA DAR WALIOPATA MIKOPO WAISHUKURU SERIKALINa Francisco Peter, Dar es Salaam

Wamachinga Dar es Salaam waliopata Fursa ya kupata Mikopo Banki wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayongozwa na Rais Dokt.Samia Sulu Hassan serikali imechochea hatua za maendeleo kwa sekta binafsi na washirika wa maendeleo katika kutengeneza mazingira wezeshi wafanya biashara ndogondogo(Wamachinga).

Wanachama hao waliojiunga na Chama cha Wafanyabiashara Ndogondogo Mkoa wa Dar es Salaam (KAWASSO) na kupata mikopo hiyo wameshukuru kwa serikali hii ya awamu ya sita kwani imeweza katika hatua hiyo ya kuweza kukopesheka.

Akizungumza juu ya mikopo hiyo Katibu wa umoja huo wa KAWASSO Agustine Choga amesema kuwa serikali imeweza kuwa mkombozi wa chama Chao.

"Ni vema kushukuru hatua za kimafanikio zinazofanywa na serikali kwania njema ya kuwakomboa wamachinga Hadi sasa fursa ya mikopo imeendelea kutufikia,"amesema Choga.

Choga amesema juhudi za serikali zinazofanyika kuanzia ngazi ya Mkuu wa Mkoa zimekuwa zikiwaongoza kwa Kila namna hadi hivi sasa mikopo hiyo imeongeza kukuwa kwa uchumi wa Machinga.

Kwa upande wa machinga Stambuly Issa ambaye ni mwanachama wa KAWASSO akiwa ni machinga aliyeji[atia mkopo wake wa Shilingi Milioni Moja mwaka jana, kupitia Maendeleo Bank ya jijini Dar es Salaam ameshukuru Serikali ya awamu ya sita kwa juhudi zinazoendelea kufanyika katika kuwakomboa kiuchumi.

"Niliweza kipata mkopo wa shilingi milioni Moja na niliweza kurudisha mkopo wote na hivi karibuni inaweza kuwa sikuchache nitapata mkopo mwingine kupitia taasisi hiyo ya kifedha,"amesema Issa.

Issa ambaye ufanya biashara ya kuuza mapazia mtaa wa Agrey na Sikukuu amefurahia sana hali nzuri ya uchapakazi ya viongozi wa KAWASSO unaoongozwa na katibu wa chama hicho Bw.Choga.

Naye mfanyabiashara mwingine wa machinga katika chama hicho Khamis Chokota akiwa ni muuza vijora katiks mtaa wa Mhonda na Raha ambaye pia ni mjumbe wa KAWASSO akiongoza wadau wasiopungua 280 ambao wete ni wamachinga amesema kuwa naye aliweza kufanikiwa kukopa Milioni Moja na kuweza kurudisha mkopo ndani ya muda elekezi .

Aidha Chokota amesema kuwa siku si nyingi atakuwa amepata mkopo mwingine utakao mwezesha kukua kimtaji na kufanya kuzidi kuchangamka kwa biasha yake.
Uongozi wa KAWASSO unajipambanua kuwa na wajumbe Katika mitaa iliyojipangia ambapo kimuongozo hali ipo shwali huku wajumbe hao wakitajwa kuwa ni wasio zidi 40 .

Post a Comment

0 Comments