Ticker

6/recent/ticker-posts

WASAFIRISHAJI WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU ILI KUFIKISHA MAZAO SOKONI YAKIWA BORA



*****************


Njombe


Wasafirishaji wa mazao ya mbogamboga yakiwemo matunda ya Parachichi mkoani Njombe wameiomba serikali kuboresha miundombinu ya usafirishaji wa bidhaa hizo ili kuweza kusafirisha zikiwa na ubora na kwa wakati.


Hayo yameelezwa katika mkutano wa uhamasishaji wa usafirishaji wa mazao lmbogamboga na matunda kwa njia ya meli na viwanja vya ndege vya ndani ya nchi ulioandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC,Taasisi ya Kikanda ya Uchukuzi ya ISCOS pamoja na Baraza la Wasafirishaji Tanzania TSC.


Akizungumza katika mkutano huo mmoja wa wasafirishaji Zekomo Masanje aliomba kuwepo kwa majokofu ya kuhifadhi baridi,bandari kavu na kuomba pia kuondolewa kwa vikwazo vya usafiri barabarani ili magari yasafiri kwa haraka.


"Changamoto kubwa ni contena za friji ambazo kwa sasa zinapatikana Nairobi kwa hiyo unakuta kuna gharama kubwa na pia hizo contena tunatumia bandari ya Mombasa ambapo unakuta kuna gharama kubwa katika usafirishaji unakuta ukikodi contena kutoka Nairobi ije Njombe,itoke Njombe iende Mombasa.Tunashauri kama kuna uwezekano serikali yetu ya ndani kwamba tuweze kuweka utaratibu mzuri kwenye bandari yetu ya Dar es salaam"alisema Masanje.


Katibu mtendaji wa baraza la usafirishaji shehena Tanzania,Sallu Jonhsons alisema changamoto kubwa inayowakabili wasafirishaji shehena ni ucheleweshaji wa usafiri wa mizigo kutoka mashambani kuelekea bandari.


"Kama bandari ya Dar es salaam,uwanja wa ndege wa Dar es salaam,uwanja wa KIA tunapata matatizo kwa sababu ya changamoto ambazo wanakutana nazo,kuna mizani kuna watu wa usalama lakini tunatizama na nafikiri ikiwezekana gari inavyotoka Njombe itapimwa uzito itakidhi taratibu zote za barabara akiwa amepata vile na kontena limepakia mzigo na afisa wa forodha amethibitisha kwamba mzigo umeingia ndani ni boksi kadhaa kadhaa akafunga siri yake na gari ikaenda ikapimwa uzito watu wa tanroad mizani wakatoa cirtificate hakuna sababu gari kuendelea kusimamishwa hadi kufika Dar es salaam ikiwa imebeba bidhaa hizi hatarishi kwa kuogopa ubora wake kuharibika"alisema Johnson.


Awali mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njonbe Antony Mtaka aliomba kuwekewa majokofu katika bandari kavu inayotarajiwa kuanzishwa halmashauri ya Mji Makambako.


"Tunampango wa kuanzisha bandari kavu Makambako ili kuhakikisha kwamba uchumi huu ambao mnauona unakuwa wa Njombe basi tunakuwa tunasehemu ambayo watu wanakuwa wanatoka nchi za jirani ambazo zimepakana na nyanda za juu kusini wafike waweke bidhaa zao zote center kubwa iwe Makambako"alisema Kasongwa.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Udhibiti wa Huduma za Usafiri kwa njia ya Maji
TASAC Deogratius Mukasa, alisema lengo la mkutano huo ni kupokea changamoto ili zikafanyiwe kazi ili kuhakikisha huduma za usafirishaji zinawafikia.


"Lengo ni kuwawezesha wasafirishaji wa ukanda huu wa nyanda za juu kusini wanaotumia huduma za bandari kusafirisha bidhaa nje ya nchi kipata uelewa juu ya namna bora ya kutekeleza majukumu yao usafirishaji kwa namna wanavyoweza kulinda maslahi yao katika kutumia huduma za usafirishaji"alisema Mukasa.


Muwakilishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini TPA Robert Soko alisema maboresho makubwa yamefanyika ili kuvutia
wasafirishaji wa mali mbichi nchini kutumia usafiri wa meli.


Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uchukuzi ISCOS Aderick Kagenzi alisema Teknolojia inatumika ili kukabiliana na changamoto za usafirishaji.


Post a Comment

0 Comments