Ticker

6/recent/ticker-posts

WASHINDI WA TUZO ZA UANDISHI BUNIFU WAPATIKANA, RAIS MSTAAFU WA MSUMBIJI APONGEZA KUANZISHWA TUZO HIZO

Mshindi wa kwanza shindano la Uandishi Bunifu katika upande wa Shairi Bw.Amri Abdallah kutoka Mkoa wa Kilimanjaro akipokea Hundi ya Shilingi Milioni Kumi (10,000,000/=) kutoka kwa mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joaquim Chissano mara baada ya kufanikiwa kushinda kupitia Shairi lake la 'Mtale wa Ngariba' kwenye hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mshindi wa kwanza Shindano la Uandishi Bunifu katika upande wa Shairi Bw.Amri Abdallah kutoka Mkoa wa Kilimanjaro akipokea cheti cha mshindi wa kwanza kutoka kwa mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joaquim Chissano mara baada ya kufanikiwa kushinda kupitia Shairi lake la 'Mtale wa Ngariba' kwenye hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mshindi wa kwanza shindano la Uandishi Bunifu katika upande wa Shairi Bw.Amri Abdallah kutoka Mkoa wa Kilimanjaro akipokea ngao ya ushindi kutoka kwa mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joaquim Chissano mara baada ya kufanikiwa kushinda kupitia Shairi lake la 'Mtale wa Ngariba' kwenye hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Mshindi wa kwanza Shindano la Uandishi Bunifu katika upande wa Riwaya Bw. Hamisi Kibali kutoka Mkoa wa Dar es Salaam akipokea Hundi ya Shilingi Milioni Kumi (10,000,000/=) kutoka kwa mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joaquim Chissano mara baada ya kufanikiwa kushinda kupitia Riwaya yake ya 'Gereza la Kifo' kwenye hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Mshindi wa kwanza Shindano la Uandishi Bunifu katika upande wa Riwaya Bw. Hamisi Kibali kutoka Mkoa wa Dar es Salaam akipokea ngao ya ushindi kutoka kwa mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joaquim Chissano mara baada ya kufanikiwa kushinda kupitia Riwaya yake ya 'Gereza la Kifo' kwenye hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mshindi wa Pili wa Shindano la Uandishi Bunifu Bw.Shaban Maulid kutoka Mkoa wa Dar es Salaam akipokea Hundi ya Shilingi milioni saba (7,000,000/=) kutoka kwa mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joaquim Chissano mara baada ya kufanikiwa kushinda kupitia Shairi lake la 'Utu bora Uzalendo kwenye hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mshindi wa Pili wa Shindano la Uandishi Bunifu Bw.Dickson Mtalaze kutoka Mkoa wa Dar es Salaam akipokea Hundi ya Shilingi milioni saba (7,000,000/=) kutoka kwa mgeni rasmi Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joaquim Chissano mara baada ya kufanikiwa kushinda kupitia Riwaya yake 'Kigodoro kimeniponza' kwenye hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mstaafu wa Msumbiji Mhe.Joaquim Alberto Chissano akizungumza katika hafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza katikahafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba akizungumza katikahafla ya Utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu inayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Johari Rotana jana Aprili 13,2023 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


*********************** 

RAIS Mstaafu wa Msumbiji Mhe. Joaquim Chissano ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuanzisha tuzo ya taifa ya mwalimu nyerere ya uandishi bunifu ambapo amesema itasaidi kuuza na kuenzi lugha adhimu ya kiswahili kwa nchi za Afrika ili kuendeleza matumizi kwenye maeneo muhimu ya kiutawala na kijamii.

Akizungumza wakati wa hafla ya Utoaji Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere Aprili 13, 2023 jijini Dar es Salaam Rais mstaafu wa Msumbiji Joaquim Chissano amesema kiswahili ni tunu na utambulisho wa afrika na mwafrika

“Juhudi za kutambua mchango wa wadau wa maandiko bunifu kwa lugha ya kiswahili ni muhimu na kwamba juhudi hizi ziendelezwe kwani uhai wa lugha yoyote duniani ni kuwapo na machapisho yaliyoandikwa kwa lugha hiyo” amesema Rais Mstaafu Chissano

“Ni wazi Mwl. Nyerere kwa dhati kabisa aliikuza lugha ya kiswahili kwa kuandika maandiko bunifu kama riwaya, mashairi na kutafsiri kazi mbalimbali za fasihi ya kingereza katika kiswahili hivyo ni heshima kubwa tuzo hii kupewa jina lake,” amesema Rais Mstaafu Chissano

Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Wizara imejipanga kuhakikisha utoaji tuzo za uandishi bunifu unakuwa endelevu na kwamba itahusisha nyanja mbalimbali ikiwemo uandishi wa vitabu vya watoto ili kujenga tabia ya watoto kujisomea wakiwa wadogo na zitakuwa zikitolewa kila mwaka Aprili 13.

Amesema lengo la tuzo hizo ni kuwatambua na kuwazawadia waandishi bunifu mahiri katika nyanja mbalimbali, kukuza lugha ya taifa ya Kiswahili, vipaji vya uandishi bunifu kwa Watanzania, kuongeza hamasa ya Watanzania kujisomea, kuhifadhi historia, amali na kukuza sekta ya uchapishaji na hifadhi za vitabu kwa shule, vyuo na maktaba zetu.

Post a Comment

0 Comments