Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA AFYA YATOA FURSA KWA MWEKEZAJI KUJENGA KIWANDA CHA MIFUKO YA KUHIFADHIA DAMU NCHINI


Na Magrethy Katengu

Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu amewaomba Wawekezaji kujitokeza kujenga Viwanda vya kuzalisha Mifuko ya kuhifadhi damu Ili kusaidia kupunguza gharama ya kuagiza nje ya nchi na Wizara itahakikisha inakuwa bega kwa bega kuhakikisha mwekezaji huyo anafanikiwa .

Ombi hilo amelitoa leo Jijini Dar es salaam wakati alipotembelea benki ya Taifa ya Mpango wa damu salama Taifa katika ziara yake aliyoifanya leo katika benki hiyo aligundua kuwa changamoto hiyo ya upungufu wa Mifuko ya kuhifadhia damu salama itatatuliwa kwa kuwepo kwa kiwanda angalau kimoja cha kuzalisha mifuko hiyo na kuacha kununua kwa kuagiza nje ya nchi

"Nawashuluru sana Wananchi wote wanaojitokeza kuchangia damu kwani ni tendo la huruma,utu,Upendo kwani wanasaidia sana makundi ikiwemo wajawazito,wanapata ajali, na watoto hivyo Benki hakikisheni mnakuwa na Mifuko ya kuhifadhia damu ya kutosha nchi nzima ibakie wananchi wenyewe kuchangia damu" amesema Waziri

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa damu Salama Tanzania Dkt Abdu Juma Bhombo amesema uratibu na usimamizi wa Mifuko ya kukusanyia damu kuna Mifuko ya kukidhi matumizi ya miezi mitatu na nusu na changamoto tuliyoipata ya ukosefu wa Mifuko ya kuhifadhia damu Bohari ya Dawa (MSD) walikuwa bado hawajaingia mikataba na wazabuni hivyo Sasa tayari wameshatoa mikataba kwa wazabuni wa kuagiza Mifuko hiyo.

"Kwa mwaka 2022/2023 tumeshatengeneza makontena ya Mifuko laki saba hamsini na Moja ambayo inakidhi matumizi ya nchi nzima ambapo matumizi ni Mifuko laki tano tisini kwa mwaka mzima kulingana na Sensa iliyofanyika mwaka 2022 ukitoa Zanzibari"amesema Dkt Bhombo

Hata hivyo amesema mahitaji ya nchi ni chupa laki tano na tisini na kwa kwa mwaka hadi kufikia Februari 2023 wamefanikiwa kukusanya damu chupa laki mbili na tisini na nne sawa na 79% Malengo waliyojiwekea walitakiwa kukusanya laki tatu na tisini na sita hivyo

Aidha amesema hali ya upatikanaji unaridhisha lakini kuna changamoto ya kundi AB,b,na 0 negative Makundi haya wachangiaji wa damu ni wachache nchi nzima waliojitokeza ni 350 na wamefanikiwa kuwaweka kwenye group moja Ili kama kukitokea uhitaji iwe rahisi mgonjwa kusaidiwa.

Aidha Wizara ya Afya kuna haja kila mtoto anayezaliwa apimwe kundi ifahamike kundi lake la damu na iwekwe kanzi data hata mtu anapoenda hospitali yeyote asipimwe na itarahisisha kujua takwimu ya watu watu wote na makundi yao ya damu miaka ijayo.


Post a Comment

0 Comments