Ticker

6/recent/ticker-posts

CHANGIA WAGONJWA WANAOUGUA SARATANI KWANI KUNA WANAOSHI MAZINGIRA MAGUMU WANAHITAJI SADAKA YAKO


Na Magrethy Katengu

Umoja wa Machifu Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Saratani Ocean Road wameandaa mechi ya mpira wa miguu kati ya Machifu na Wabunge wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania lengo likiwa kukusanya Milioni 300 kwa ajili ya kusaidia wagonjwa 100 wa saratani walio katika Mazingira magumu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage amesema kwa mujibu wa takwimu za julai 2022- machi 2023 inaonyesha inaonyesha hadi sasa inapata wagonjwa wapya kwa mwaka 42,046 huku saratani zinazoongoza ni pamoja ikiwemo saratani ya shingo ya kizazi, (44%,) matiti(17%,)njia ya chakula koo (12%) kichwa na shingo(9%)Kaposi sarcoma(6%)tezi dume (5%)utumbo mpana(2%)thyroid(3,%)lymphoma(1%) saratani ya damu(1%)

"Kotokana na hali ya familia nyingi zenye wagonjwa wa saratani huathirika zaidi kwa sababu hulazimika kusafirisha wagonjwa wao kutoka sehemu mbali hadi taasisi ya ocean road hulazimika kutafuta hifadhi kwa ndugu na wengine wakikosa hulala nje huku baadhi yao wakishandwa gharama hutelekeza wagonjwa wao hospitali serikali huwasaidia kupata msamaha nauli za kurudi makwao huingia Mtaani na kuwa ombaomba "amesema Dkt

Dkt Mwaisalage amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali na wadau mbalimbali bado changamoto ni kubwa kwani wagonjwa wanahitaji mahitaji makubwa yakiwemo ya kimatibabu ili wapate huduma nzuri na kuweza kuendelea kuzipigania ndoto za maisha yao hivyo kupitia kuchangia itasaidia wanafamilia ndugu, jamaa kupunguziwa mzigo

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Machifu Tanzania kutokea Mkoa wa Simiyu Antonia Sangalali amesema wamepanga Mtanange huo wa mpira wa miguu kurindima Jijini Dodoma katika uwanja wa Jamuhuri Mei 27 ambapo machifu wataanza kuwasili mei 25 mwaka. huu hivyo Wananchi na watu binafsi wachangie fedha zao za kusaidia wanaugua saratani kipitia ACCOUNT YA NMB NO 20101100166 ambayo inamilikiwa na Ocen road na fedha za zitafika moja kwa moja na kufanya mlengo uliokusudiwa .

Aidha Magonjwa ya saratani hayana hodi na hayachaguai familia na huwezi kupanga lini unaingia na lini unatoka ni wajibu wa jamii kufanya kila linalowezekana kuzisaidia jamii zenye changamoto ili kupunguza ugumu na machungu wanayopitia

Post a Comment

0 Comments