Ticker

6/recent/ticker-posts

PROF.NDALICHAKO:BILIONI 3 ZIMETOLEWA KUJENGA VYUO VITATU VYA WATU WENYE ULEMAVU 


Na Mwandishi Wetu, Kasulu 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako amesema Sh.Bilioni tatu zimetolewa na serikali kwa ajili ya kujenga vyuo vitatu vya watu wenye ulemavu na utegamano.

Vyuo hivyo vinajengwa na serikali kupitia Ofisi hiyo kwenye Mikoa ya Songwe, Ruvuma na Kigoma na tayari kila chuo kimepewa Sh.Bilioni moja ili kujenga madarasa, mabweni na nyumba za walimu.

Akizungumza Mei 27, 2023 alipokagua ujenzi wa chuo kinachojengwa eneo la Nyumbigwa, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambacho ni miongoni mwa vyuo hivyo, Prof.Ndalichako amesema kujengwa kwa vyuo hivyo ni msisitizo wa serikali kwenye mafunzo ya ujuzi kwa watu wenye ulemavu.

“Nimshukuru kwa dhati Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kusogeza huduma kwa jamii katika maeneo muhimu. Tuna chuo cha mazoezi Kabanga kina wanafunzi wengi wenye ulemavu,”amesema.

Post a Comment

0 Comments