Ticker

6/recent/ticker-posts

SENYAMULE AKABIDHI TUZO YA PONGEZI FOUNTAIN GATE PRINCESS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewakabidhi Tuzo ya pongezi timu ya wasichanana ya Fountain gate kwa kutwaa Ubingwa wa Mashindano ya Shule za Sekondari za wasichana Afrika yaliyofanyika Nchini Afrika kusini yakihusisha Shule zote za Sekondari kupitia Kanda ambapo timu hiyo ilishiriki kupitia kutwaa Ubingwa wa CECAFA ikiwa ni Ukanda wa Afrika Mashariki.

Hafla ya makabidhiano ya Tuzo imefanyika katika Ukumbi wa Landmark hotel jijini Dodoma ambapo imeambatana na chakula cha mchana kilichowajumuisha watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Timu ya wasichana ya Fountain Gate, Wakurugenzi wa Halmashauri za Dodoma pamoja na wawakililishi kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

"Mmetufurahisha kuifanya Dodoma ya Utalii wa michezo, watu wanakuja kuwapongeza mnaongeza upana wa ushirikiano sio tu katika michezo bali hata katika biashara na sisi Kama mkoa tutawapa ushirikiano wa kila aina sio tu katika michezo Ila hata kwenye Elimu na mnafanya vizuri pia niwatakie kila la kheri katika masomo yenu na kuendeleza vipaji vyenu.

"Tunafurahi mna malengo ya kujenga viwanja vya mpira hapa na kama mnavojua Serikali ina malengo ya kujenga Arena hapa kwa hiyo mnaenda sambamba na maono ya Serikali Jambo ambalo mtasaidia kukuza uchumi wa Taifa kupitia sekta ya Michezo" amesisitiza Mhe. Senyamule

Aidha Meneja wa Kitengo cha Mahusiano cha Fountain Gate Bw. Denis Joel amesema kupitia mashindano hayo wamefanikiwa kupata ufadhili wa kimasomo kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha Nne pamoja na baadhi ya wachezaji kupata timu zinazoshiriki ligi mbalimbali ikiwemo Laliga.







Wajumbe wa Kikao Kamati ya Wataalamu wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula (LDFS) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakijadili taarifa ya utekelezaji wa Mradi katika kipindi cha Julai 2022- Machi 2023. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma, Mei 12, 2023.





Wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Wataalamu wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula (LDFS) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyojadiliwa wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mji wa Serikali, Mtumba Dodoma, Mei 12, 2023.

Post a Comment

0 Comments