Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO AZINDUA MIRADI MVOMERO, AWATAKA WANANCHI KUITUNZA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewataka wananchi kulinda miradi ya maendeleo, hifadhi ya mazingira kwa kupanda miti pamoja na kulinda uoto wa asili ili iendelee kudumu.

Ametoa rai hiyo leo Mei 03, 2023 wakati akizindua miradi mbalimbali kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

Dkt. Jafo amezindua miradi hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 520 ikiwemo uchimbaji wa visima viwili virefu vya maji inayojumuisha mfumo wa sola kwa ajili ya kuvuta maji, matanki ya kuhifadhi maji pamoja na mfumo wa umwagiliaji na wa matumizi ya wananchi, lambo la lenye uwezo wa kukusanya maji lita za ujazo 252,299 zikiweza kumwagilia hekta 287 za mazao ya mbogamboga, kiwanda kidogo cha sabuni na kikundi cha uzalishaji uyoga.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vilivyonufaika na mradi vya Melela, Magali na Mingo, amesema kuwa Serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha wananchi katika maeneo yenye ukame wanapata mafanikio.

Amesema Serikali inapeleka miradi kwa wananchi ili kuwasaidia katika kupata fursa za kimaendeleo pamoja licha ya kuwepo kwa changamoto za mabadiliko ya tabiachi zinazochangia ukame.

“Ndugu zangu niwashukuru sana kwa kutekeleza hii miradi na niwaombe tuilinde asitokee mharibifu akaja kuharibu miundombinu tumsimfumbie macho, lakini pia ajenda yetu kuu tutunze mazingira, usipoyatunza na kuyashughulikia mazingira yatakushughulikia”, amesisitiza.

Kutokana na hali hiyo hivyo, Dkt. Jafo amewapongeza viongozi katika wilaya hiyo kwa usimamizi mzuri wa miradi na kuwa wananchi wanaponufaika nayo ni jambo jambo la heri.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Judith Nguli amemshukuru Waziri Jafo kwa kutembelea wilaya hiyo na kuzindua miradi hiyo kwa manufaa ya wananchi.

Mkuu wa wilaya huyo ameahidi kwa kushirikiana na timu yake kuisimamia na kuilinda miradi hiyo ya maendeleo kwa nguvu zote kuhakikisha inakwenda kwa wananchi kama ambavyo Serikali inaagiza.

Aidha, Mhe. Judith amesema wilaya yake inatekeleza shughuli za hifadhi ya mazingira ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa kuhakikisha inatoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira.

Baadhi ya wananchi wakiwemo Bw. Fortunata Mathias, Said Salum na Mohamed Seif Diwani wa Kata ya wameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuwapelekea Mradi wa EBARR.

Wsmesema kuwa kupitia mradi wa vitalu nyumba vilivyozinduliwa wataweza kujihusisha na kilimo cha mbogamboga hivyo kujipatia kipato tofauti na hao awali amapo walishindwa kufanya shughuli za kilimo wakati wa kiangazi.

“Sisi wa wakulima tuliteseka sana kutokana na shida ya maji iliyosababishwa na ukame lakini sasa hivi tunafanya kazi vizuri tunamwagilia mazao yetu, tunaomba Serikali iongeze mabwawa ili tuweza kulima Zaidi,” amesema.

Mradi wa EBARR unatekelezwa pia katika Wilaya ya Simanjiro (Manyara), Mvomero (Morogoro), Kishapu (Shinyanga) na Kaskazini ‘A’ Unguja (Zanzibar) chini ya ufadhili wa Mfuko wa Mazingira wa Dunia chini ya Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Mingo wakati wa ziara ya kukagua na kuzindua miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Mei 03, 2023 ambapo ametoa wito kwa wananchi kuitunza miradi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikagua lambo lambo la lenye uwezo wa kukusanya maji lita za ujazo 252,299 Kijiji cha Melela baada ya kuzindua mradi huo kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Mei 03, 2023 ambapo ametoa wito kwa wananchi kuitunza miradi hiyo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizundua mradi wa maji katika Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Mei 03, 2023 ambapo ametoa wito kwa wananchi kuitunza miradi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikagua kitalu nyumba ambacho kimejengwa sambamba na kisima cha maji kinachojumuisha mfumo wa sola kwa ajili ya kuvuta maji, matanki ya kuhifadhi maji pamoja na mfumo wa umwagiliaji na wa matumizi ya wananchi, wakati wa ziara yake ya kuzindua Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Mei 03, 2023 ambapo ametoa wito kwa wananchi kuitunza miradi hiyo. Katika ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Mhe. Judith Nguli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipanda mti katika Kijiji cha Melela wakati wa ziara ya kukagua na kuzindua lambo lambo la lenye uwezo wa kukusanya maji lita za ujazo 252,299 Kijiji cha Melela baada ya kuzindua mradi huo kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Mei 03, 2023 ambapo ametoa wito kwa wananchi kuitunza miradi hiyo.
Kitalu nyumba ambacho kilichojengwa sambamba na kisima cha maji kinachojumuisha mfumo wa sola kwa ajili ya kuvuta maji, matanki ya kuhifadhi maji pamoja na mfumo wa umwagiliaji na kwa matumizi ya wananchi kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Mei 03, 2023 ambapo ametoa wito kwa wananchi kuitunza miradi hiyo.
Mradi wa kisima cha maji kinachojumuisha mfumo wa sola kwa ajili ya kuvuta maji, matanki ya kuhifadhi maji pamoja na mfumo wa umwagiliaji na kwa matumizi ya wananchi kupitia Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Mei 03, 2023 ambapo ametoa wito kwa wananchi kuitunza miradi hiyo.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Post a Comment

0 Comments