Ticker

6/recent/ticker-posts

WHMTH YAPOKEA UGENI WA WATANGAZAJI WA KIPINDI CHA GOOD MORNING CHA WASAFI MEDIA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amepokea ugeni wa watangazaji wa kipindi cha Good Morning cha Wasafi Media wakiongozwa na Mkuu wa Vipindi vya Wasafi FM, Nelson Kisanga, kwa upande wa Watangazaji ni Bw. Gerald Hando, Hillary Daudi Mtuta (Zembwela) na wengineo na kufanya nao mazungumzo mbalimbali ya sekta ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA, Mei 04, 2023 jijini Dodoma.

Ugeni huo ulipata pia wasaa wa kutembelea jengo jipya la ofisi za Wizara linalojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Watangazaji hao walipongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kuendelea kutekeleza maazimio yaliyoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu ya Serikali katika kipindi cha miaka ya 1970.

Ugeni huo ulihudhuriwa pia na Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.


Post a Comment

0 Comments