Ticker

6/recent/ticker-posts

FCC KUFANYA MAADHIMISHO YA BIDHAA BANDIA JUNI 8-15 MWAKA HUU DODOMA*********************

Na Magrethy Katengu

Tume ya Taifa ya ushindani nchini FCC inatarajia kufanya maadhimisho ya June 8-15 mwaka huu ambapo na kilelele chake kitafanyika Dodoma wiki hiyo ikiambatana na kutoa elimu kwa Wananchi namna ya kuepukana bidhaa bandia.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa tume ya ushindani FCC William Erio amesema kuwepo kwa bidhaa bandia zina athiri soko la ushindani ni uvunjifu WA Sheria kwani linaathiri soko na watumiaji hivyo katika wiki hiyo watatoa Elimu kwa wananchi .

"Jukumu la tume ya ushindani nchini (Fcc) nikulinda bidhaa ya uchumi na kumlinda mlaji athari kwani bidhaa bandia zina athari kubwa kwa jamii lakini imekuwa mazoea na wakienda kununua bidhaa huuziwa pasipo risiti na huuzwa bei ya chini hivyo pasipo kufahamu kuwa ina madhara gani" ".Alisema Mkurugenzi Mkuu Fcc William Erio

Mkurugenzi wa Fcc William Erio amesema zoezi la maadhimisho la wa bidhaa bandia yatataongozwa na kauli mbiu "Kukuza ubia kati ya sekta ya Umma na sekta binafsi kupambana na bidhaa bandia " hivyo katika mwaka 2022/2023 robo ya mwaka alivyofanya wa ukagua mizigo bandarini makasha 4700 bidhaa bandia 58ndio zilikutwa hazina viwango na ziliteketezwa .

Aisha Sheria ya bidhaa bandia. duniani ambapo maadhimisho hayo Kitaifa yanatarajiwa kufanyika juni 8 hadi 15 mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Dk Ashatu Kijaji Waziri wa viwanda na Biashara huku kaulimbiu ya kukuza ubia sekta ya umma na sekta binafsi katika kupambana na bidhaa bandia watu wote wanakariboshwa.Post a Comment

0 Comments